Jumatano, Aprili 30, 2014

DIAMOND NA WEMA HATARI, MAHABA HADHARANI NA DENDA NJE NJE!! HABARI NA PICHA VIKO HAPA

MASUPASTAA ambao ni wachumba (wanasema wenyewe), Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu na Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, walijikuta wakionesha upendo wao mbele za watu kwa kudendeka  barabarani.
Ishu hiyo ambayo wapendanao wengi huifanya kwa faragha, ilijiri hivi karibuni maeneo ya Bamaga- Mwenge jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo, Wema alikuwa kwenye shughuli zake za kila siku maeneo hayo ambapo alikuwa ameegesha pembeni gari lake la rangi ya pinki aina ya Toyota Lexus Harrier bila kujulikana alikokuwa ameelekea.

Ikadaiwa kuwa, mara Diamond naye alitokea bila kujulikana alikotokea akiwa anaendesha gari lake aina ya Toyota Prado na kuegesha gari lake jirani na alipoegesha Wema.
Kweli, lilikuwa tukio lilionesha kushangaza kwani shuhuda alikuta wapita njia wakiwa wanapunguza mwendo ili kuwashuhudia wawili hao walichokuwa wakikusudia kukifanya bila kuogopa watu. 
Kamera iliweza kuwanasa wawili hao, Wema yeye alisimama nje ya gari la Diamond upande wa dirisha la dereva na kuongea na mwandani wake huyo jambo ambalo hakuna mpita njia aliyeonekana kushangaa.

Hata hivyo, mshangao ulianza pale Diamond alipotoa mkono nje na kumshika kiuno Wema huku wakiendelea kuongea ndipo baadhi ya wapita njia nao walipokoleza macho kodo, wengine wakihoji kama aliyesimama nje ya gari ni Wema, nani alikuwa ndani ya gari hilo!

Haikuwa rahisi kupata majibu kwani wengi walikuwa wanashindwa kumwona Diamond. Wengine waliamini kwamba, Wema alikuwa ameshikwa kiuno na mwanaume mwingine ambaye huena akampindua Diamond kama na yeye alivyompindua yule kigogo wa ikulu ‘CK’.

Sasa mbona Wema anakubali kushikwa kiuno hivihivi tu, haoni watu?
alihoji mpita njia mmoja ambaye alijitambulisha kwa jina la Salome, mwanafunzi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama jijini Dar.
Katika hali isiyotarajiwa, baada ya kushikwa kiuno, Wema alikwenda mbali zaidi pale alipomwinamia ‘baby’ wake huyo na kula naye denda ambapo naye mwanaume hakufanya ajizi hata kidogo.
He! Jamani! Naona wenzetu leo wameamua, hata barabarani? Huu ustaa nahisi unawafanya watu wawe vichaa mbele za watu. Mimi siwezi kabisa kudendeka mbele za watu,
alisema mrembo mmoja ambaye hakutaka kutaja jina lake lakini naye ni denti wa Chuo cha Ustawi wa Jamii ambacho kipo jirani kabisa na eneo la tukio.
Baada ya denda hilo lililodumu kwa dakika moja, Diamond alimuaga Wema na kukanyaga mafuta kuondoka katika eneo hilo huku wananachi wakimfuatilia kwa macho yaliyojaa mshangao.

0 comments:

Chapisha Maoni