Jumatano, Aprili 30, 2014

NEY WA MITEGO AKANUSHA KUTISHIA KUUA

Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ amefungukia skendo ya kumtishia kumuua mdogo wake aitwaye Amani Shija.
Nay alisema kwamba anasikitishwa sana na malalamiko hayo kwani katika maisha yake hajawahi kumtishia mtu kumuua na hajui ni kipi ambacho kimemvuta hadi kuanza kulalama mambo kama hayo

Hakuna ishu kama hiyo, kwanza Amani siyo ndugu yangu wa damu ila udugu wangu naye niliutengeneza baada ya kukutana naye Ubungo miaka minne iliyopita na akaniomba nimsaidie, bila kinyongo nilianza kuishi naye hadi leo hii anaanza kunitolea maneno kama hayo
alifafanua Nay na kuongeza:
Ameshindwa kujielewa lakini mimi namuachia Mungu maana kama kumsaidia nimeshamsaidia sana, nshamlipia hadi chumba zaidi ya miaka minne na nikamtimizia mahitaji yake yote, lakini wapi.

0 comments:

Chapisha Maoni