Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mbeya
(Must), Scholastica Loppa anasema asilimia kubwa ya wanawake au
wasichana wanaosoma sayansi ni wazuri na hawazeeki.
Akiwa ndani ya mavazi ya kawaida, mweupe kwa rangi
ya mwili huku kichwa chake kikiwa kimesheheni nywele nyeusi za asili
zisizo na hata chembe ya kemikali, Loppa alikuwa na mengi ya kuwaeleza
waltu.
Masomo ya sayansi hayazeeshi si mnaniona mimi hapa? Napendeza, sipendezi?alihoji mhadhiri huyo mbele ya umati uliofika kwenye chuo hicho kushuhudia uzinduzi wa kampeni za kuhamasisha wasichana wasome masomo ya uhandisi na teknolojia (Wited).
Kampeni hiyo inaratibiwa na chuo hicho kupitia
mpango maalumu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola Afrika wa kuhimiza
wasichana wasome sayansi na ufundi.
Mhadhiri huyo aliwasihi wasichana wa sekondari na
vyuo mbalimbali nchini kutosikiliza madai kuwa wanawake wanaosoma
sayansi wanazeeka mapema, kwa sababu masomo hayo yanahusisha kufikiri
kwa kiwango kikubwa.
Aungwa mkono
Kauli imepokelewa kwa mikono miwili na baadhi ya
watu, akiwamo mkurugenzi msaidizi wa Wizara ya Sayansi na Teknolojia,
Margreth Komba anayesisitiza kwamba wanawake waliosoma sayansi wanaishi
maisha ya raha zaidi kuliko wanaosoma fani nyingine.
Anaeleza kuwa masomo ya sayansi kwa wanawake
yanawaongezea maarifa zaidi, kwani wao wamezaliwa kisayansi zaidi na
ndio maana wanafanya kazi nyingi zikiwamo za kutumia moto jikoni.
Naye Mwenyekiti wa mpango huo chuoni hapo na
mhadhiri wa sayansi na biashara, Albertina Leonard, anasema wanawake ni
kila kitu katika maisha duniani.
Anasema uzinduzi wa mpango wa Wited ni ukurasa
mpya kwa chuo hicho kuanzisha kampeni maalumu kuwahamaisha wanawake
walio kazini na hata wanafunzi wa sekondari kujipanga kupenda masomo ya
uhandisi na teknolojia.
Tutakwenda kwenye shule mbalimbali kuwahimiza wasichana wasome sayansi
Naye Mhandisi Eunice Maonyesho, anasema:
Wasichana au wanawake wote wanaweza kusoma na kufaulu vizuri sayansi kuliko wanaume. Mimi naamini hivyo kwa sababu wasichana walioamua tangu mwanzo walifanikiwa.
0 comments:
Chapisha Maoni