Miaka 104 iliyopita siku kama leo, aliaga dunia akiwa na umri wa miaka
67 Robert Koch, mgunduzi wa vijidudu maradhi aina ya bakteria na tabibu
mashuhuri wa Kijerumani aliyegundua chanzo cha maradhi ya kifua kikuu au
TB. Daktari Robert Koch alianza kutwalii na kufanya utafiti mkubwa juu
ya sababu au vyanzo vya kutokea baadhi ya magonjwa kama vile
kipindupindu, kimeta na kifua kifuu, baada ya kuhitimu masomo yake
katika fani ya tiba. Mwaka 1882 Miladia, Robert Koch alifanikiwa
kugundua vijidudu maradhi vinavyoitwa mycobacterium tuberculosis
vinavyosababisha kifua kikuu. Ili kukamilisha uchunguzi wake tabibu huyo
Mjerumani alisafiri katika nchi za Afrika Kusini, Misri na India na
kutwalii magonjwa mengineyo maarufu katika maeneo hayo kama vile
Malaria. Mwaka 1905 Robert Koch alitunukiwa Tunzo ya Nobel katika uwanja
wa Tiba.
0 comments:
Chapisha Maoni