Miongoni mwa changamoto kubwa iliyopo sasa katika nchi
zilizoendelea na zinazoendelea kwa watumiaji wa simu za mikononi ni
kupotewa na simu zao ama kuibwa.
Takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 56 ya watumiaji
wa vifaa vya mawasiliano duniani hupoteza simu na kompyuta mpakato kila
mwezi. Nchini Marekani pekee kila baada ya dakika moja simu 113 hupotea
ama kuibwa.
Wakati tatizo la wizi wa simu na tabiti
likiendelea, watengenezaji wa vifaa hivyo hawako nyuma, nao sasa
wanabuni teknolojia zinazomwezesha mmiliki kukipata kifaa chake
kilichopotea au kuibwa.
0 comments:
Chapisha Maoni