KUFUATIA uongozi wa Azam fc kumsainisha mkataba wa miaka miwili
kiungo mkabaji wa Yanga sc, Frank Domayo `Chumvi` akiwa katika kambi ya
Taifa ya Tanzania, mwanasheria na wakala wa kimataifa wa wachezaji
anayetambuliwa na shirikisho la soka duniani FIFA, Dkt. Damans Ndumbaro
amesema hakuna sheria inayozuia mchezaji kusainishwa mkataba akiwa kambi
ya timu ya Taifa.
Akizungumza na mtandao huu, Ndumbaro amesema sheria inaeleza kuwa mchezaji anayetakiwa kusajiliwa na timu ni yule aliye huru baada ya kubakiza miezi sita katika mkataba wake au ana mkataba, lakini klabu inayomhitaji imezungumza na timu inayommliki mchezaji.

Domayo ni mchezaji huru na alikuwa huru kwenda klabu yoyote
Alisema Ndumbaro.
Pia alisema hakuna sheria inayosema kambi ya timu ya Taifa ni eneo linalozuiliwa watu kwenda.
Pia alisema hakuna sheria inayosema kambi ya timu ya Taifa ni eneo linalozuiliwa watu kwenda.
Kambi ya timu ya Taifa watu huwa wanaenda. Kumbuka Yondani alisajiliwa Yanga akiwa timu ya taifa, na hatukusikia mzozo wowote kwasababu hakuna kununi inayozuia hilo
Kama mchezaji ametoroka kambini ataadhibiwa kwa utoro, lakini kambi ya timu ya taifa ni sehemu ya wazi na watu wanaruhusiwa kwenda pale na huwezi kukataza watu kwenda pale
Kumbuka timu inakaa hotelini na hoteli huwa hawakai wachezaji tu, kila mtu anaweza kukaa paleAlisema Ndumbaro.
Kutokana na tukio lililotokea Aprili 30 mwaka huu kwenye kambi ya timu ya Taifa (Taifa Stars) iliyopo Tukuyu mkoani Mbeya likihusisha usajili wa Frank Domayo, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemteua Wakili Wilson Ogunde kuchunguza mlolongo mzima wa tukio hilo.
Baada ya kukamilisha uchunguzi wake, Wakili Ogunde ataishauri TFF kuhusu hatua za kisheria na kikanuni za kuchukua.
TFF ilitoa wito kwa wachezaji, klabu na wadau wa mpira wa miguu kufuata kanuni na taratibu katika utendaji wao.
0 comments:
Chapisha Maoni