DUNIA imeshavua nguo na sasa kilichobaki ni ufirauni.
Atakayekwenda kushuhudia fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil
atakumbana na mabadiliko makubwa ya maisha ya kidunia nchini humo.
Wanawake malaya nchini humo wamekubaliana na benki
za nchini humo kupata malipo kutoka kwa wateja wao kupitia kadi maalumu
za malipo za wateja hao, Credit Card. Wamepewa mashine maalumu za
kuwatoza wateja wao ambao hawana fedha mfukoni lakini wanazo katika kadi
zao za benki.
Wanawake katika mji wa Belo Horizonte uliopo maili 270 kutoka katika Mji Mkuu wa Brazil, Rio de Janeiro wamefurahishwa na kaulimbiu ya mtindo huo wa malipo ambao umepachikwa jina la “Furahia sasa, lipia baadaye”.
Wanawake katika mji wa Belo Horizonte uliopo maili 270 kutoka katika Mji Mkuu wa Brazil, Rio de Janeiro wamefurahishwa na kaulimbiu ya mtindo huo wa malipo ambao umepachikwa jina la “Furahia sasa, lipia baadaye”.
Cida Vieira, malaya wa kundi la makahaba
linalofahamika kama Aprosmig, ambaye pia ni Rais wa Chama cha Malaya
katika jimbo la Minas Gerais alidai kwamba kwa sasa hakutakuwa na
kukabana koo dhidi ya wateja ambao hawana pesa mifukoni lakini wanazo
katika akaunti zao.
Wateja wanaotaka kuendelea na starehe zao lakini hawana pesa taslimu mifukoni, wanaweza kuendelea kula raha bila ya kuingiliwaalisema Cida ambaye ni malaya maarufu wa maeneo hayo.
Kwa mujibu wa kundi hilo, wamedai kwamba malipo ya
kupitia kadi yanaleta usalama kwa mteja na vilevile taarifa za matumizi
ya mteja hazitaeleza sababu hasa za matumizi yake katika pesa
zilizotoka kwenda kwa malaya.
Wakati michuano hiyo ikiwa imebakisha siku chache
kuanza huku ligi mbalimbali barani Ulaya zikiwa zinafikia ukingoni,
baadhi ya malaya wameanza kujifunza lugha ya Kiingereza kwa ajili ya
kunasa wateja ambao hawafahamu lugha ya Kireno.
Tangu mwaka jana, malaya hao wa Brazil wamekuwa
wakijiunga katika madarasa mbalimbali ya Kiingereza nchini humo kwa
ajili ya kujifunza lugha hiyo ambayo itawarahisishia majadiliano na
wateja wao wanaotumia lugha ya Kiingereza.
Hii ni muhimu kwa heshima ya ya kazi hii. Wanawake wanapaswa kujadiliana bei na mteja na kujitetea wenyewealiongeza Cida. Umalaya umehalalishwa nchini Brazil na wanawake nchini humo wanatazamia mapato makubwa wakati wa Kombe la Dunia.
Kundi hilo la malaya pia linatazamia kujifunza
lugha mbalimbali wakiwa darasani kama vile Kihispaniola, Kiitaliano,
Kifaransa na hata Kireno kwa malaya ambao wamezamia nchini humo, lakini
hawaifahamu lugha hiyo inayotumiwa zaidi na Wabrazili.
Mpaka Juni mwaka jana, Vieira anadai malaya 20 walikuwa
wamejiunga katika madarasa hayo, lakini alikuwa anatazamia kuwa malaya
wengine 300 wangejiunga katika kundi lao lenye malaya 4,000.
Waingereza waonywa na polisi wao
Polisi nchini Uingereza imewaonya mashabiki wa
soka nchini humo kuwa Polisi wa Brazil wanawasubiri kwa hamu mashabiki
ambao watafanya ngono na watoto wadogo nchini humo kwa ajili ya
kuwapeleka jela.
Mashabiki hao wa England wameambiwa kuwa watazamie
vifungo vya gerezani nchini Brazil au Uingereza kwa kufanya ngono na
watoto wadogo ambao wamekuwa tatizo kubwa katika nchi hiyo ya Amerika
Kusini.
Ripoti kutoka Brazil zinadai kuwa watoto wenye
umri mdogo hata wa kufikia miaka 11 huwa wanavaa nguo ambazo zinawafanya
waonekane wakubwa kwa ajili ya kufanya biashara ya ngono. Ni marufuku
nchini humo kulipia huduma ya ngono kwa msichana mwenye umri chini ya
miaka 17.
Michuano ya Kombe la Dunia mwaka huu, pamoja na
ile ya Olimpiki miaka miwili ijayo inatazamiwa kufichua kwa kiasi
kikubwa tatizo hili na polisi pamoja na vyombo vya dola nchini humo
vimejipanga kuchukua hatua madhubuti.
Brazil inashika nafasi ya pili nyuma ya Thailand kwa biashara ya ngono kwa watoto.
Watoto wa Brazil wanaweza kuathirika kwa kiasi kikubwa na biashara ya ngono na wanaweza kujibadilisha hili waonekane wakubwa kuliko umri wao halisialisema Johnny Gwynne, ambaye ni mkubwa kitengo cha kuzuia masuala hayo.
Uhalifu wa ngono unatajwa kuwa wa pili kwa ukubwa
nchini humo huku waathirika wakubwa wakiwa watoto wenye umri kati ya
miaka 10 hadi 14. Zaidi ya wageni 600,000 wanatazamiwa kuhudhuria
fainali za Kombe la Dunia nchini humo ambalo linatazamiwa kuanza Juni
12.
0 comments:
Chapisha Maoni