Ijumaa, Mei 02, 2014

AUNT EZEKIEL AKALIA MOTO, MASHEMEJI WAMUANDALIA TALAKA, NI BAADA YA KUSTAREHE WAKATI MUMEWE ANASOTA JELA

Awali, ilidaiwa kuwa, Aunt aliondoka  Bongo kwenda Dubai kuungana na mumewe katika ndoa, lakini vyanzo vya karibu vikahoji mumewe yupi? Mbona yuko jela baada ya kudakwa kwa kuishi kinyume cha sheria!
Kwa mujibu wa chanzo hicho, taarifa za mumewe kuwa jela,  Aunt alizichukulia poa kwani baada ya tu ya habari hizo Aunt aliendelea kujirusha katika kumbi tofauti jijini Dar na hata nje ya Dar kana kwamba hakuna kitu kilichotokea.
Aunt Ezekiel akistarehe Dubai
Aunt hakushtuka chochote taarifa zilimfikia mapema, lakini hakuchukua hatua yoyote hata kule kuonesha kwamba amehudhunika
kilisema chanzo hicho na kuongeza:
Kama hamuamini tembeleeni katika kumbi za starehe kila siku tunakula naye bata kama kawaida, angekuwa mwingine angejaribu hata kuwa karibu na ndugu wa mume kushirikiana na kujua taarifa za mumewe.
Aunt alipoulizwa kuhusiana na taarifa hizo, alikiri kuzifahamu lakini akafafanua kuwa mumewe alikamatwa na kuachiwa huru lakini watu wa karibu wameendelea kupinga.
Mume wangu amekamatwa ndiyo lakini si kama watu wanavyosambaza maneno wanayoyajua wao na kupindisha ukweli, alikamatwa kutokana na suala la kibali cha makazi kwisha muda wake lakini amesharekebisha, ameachiwa
alisema Aunt.
Aunt Ezekiel na Demonte siku ya harusi yao
Licha ya Aunt kudai mumewe huyo alikamatwa na kuachiwa, lakini tangu alipotamka kauli hiyo mwishoni mwa mwaka jana hadi sasa, mwanaume huyo hajawahi kuonekana hadharani.
Tangu alipokamatwa hakutoka tena na ishu yenyewe aliyokamatwa nayo inasemekana ni mbaya hivyo si rahisi kutoka
kilisema chanzo hicho bila kufafanua ni ishu gani.
Wakati taarifa hizo zikiendelea kusambaa jijini Dar, staa huyo aliwahi kunaswa katika viwanja tofauti vya starehe kwenye miji ya Arusha na Dar es Salaam.
Uchunguzi wa mapaparazi wetu ulionesha kuwa kabla na baada ya taarifa za mumewe kukamatwa kusambaa, Aunt hakuonesha tofauti, aliendelea kula kunywa na kucheza kama kawaida.
Mapama wiki hii, Aunt ambaye yupo Dubai aliposti picha katika mtandao wake wa Instagram na kuonesha jinsi gani anakula raha huko.
Picha hizo zinamuonesha mrembo huyo akiwa katika bwawa maalumu la kuogelea (swimming pool) huku akinywa vinywaji tofauti hali ambayo ilileta tafsiri kwa mashabiki wake kwamba ni kuponda raha huku mumewe akidaiwa kuwa jela.
Aunt Ezekiel na Demonte katika pozi la kimahaba
Sasa huyu (Aunt) jamani vipi, badala apambane kujua hatima ya mumewe yeye yupo bize kula raha za mjini utadhani ana furaha
alichangia shabiki wake mtandaoni.
Taarifa zaidi zimeeleza kuwa mara baada ya kuzagaa kwa picha hizo katika mitandao ya kijamii, baadhi ya mashemeji wa Aunt walikuja juu na kudai wanamshangaa ni vipi haoni hali ilivyo na hawamsikii akizungumzia lolote kuhusu ndugu yao.
Mashemeji zake wamekasirika kwelikweli kwani kuzagaa kwa picha hizo mtandaoni kunaleta tafsiri kwamba Aunt hana mpango na Demonte
kilisema chanzo.
Katika kusaka data zaidi za ndugu wa Demonte, paparazi wetu alimtafuta mmoja wa mashemeji hao wa Aunt ambaye hakutaka jina lake lichorwe gazetini ambapo alisema wamechukizwa na picha hizo na wanajipanga kumpa talaka.
Huu si ubinadamu hata kidogo, sasa kwa kuwa ameamua kumwaga mboga sisi tutamwaga ugali, dawa yake tunamuandalia mipango ya talaka ambapo tukimpata Demonte kwa njia yoyote na akabariki talaka, tunampa muda wowote
alisema shemeji huyo huku akikiri kuwa hata wao hawajui Demonte yukoje kwa sasa baada ya kupoteza mawasiliano naye.

0 comments:

Chapisha Maoni