Jumanne, Mei 27, 2014

SIJUI TUNDU LISU ANAYATOA WAPI HAYA, LAKINI KAMA NDIVYO YALIVYO...POLE KWAO CCM

Msomaji wa FTZ, leo nilipokuwa nikitembelea accounts zangu katika social networks nimekutana na hii post ya Tundu Lissu, sijui kayatoa wapi lakini kwa haya...CCM hawana chao, nainukuu kama ilivyo post yake:

Katiba ya CCM inambeba Lowassa, Rostam, Chenge na kuwatosa wanafiki Membe na Sitta
Wakuu nimeipitia kwa umakini katiba ya CCM na nimegundua inamapungufu makubwa na inalinda na kuruhusu wahalifu kushika nyadhifa hata kama walishakwenda jela maisha, ilimradi tu uifurahishe kamati kuu.
Nimejaribu kuchukua sehemu ya Wanachama na viongozi katika katiba hiyo toleo la 2005.
2.1. WANACHAMA NA VIONGOZI
FUNGU LA 1:
6.Kila mtu aliyekuwa mwanachama wa TANU au wa ASP mara kabla ya kuvunjwa kwa Vyama hivyo, na aliyekuwa anatimiza masharti ya Uanachama wake, atakuwa mwanachamaa wa Chama Cha Mapinduzi, isipokuwa kama atakataa mwenyewe.
7.Raia yeyote wa Tanzania mwenye umri usiopungua miaka 18, anaweza kuwa Mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi iwapo anakubali Imani, Malengo na Madhumuni ya CCM.
8.Mtu atakayekubaliwa kuingia katika CCM, au kuendelea kuwa Mwanachama, ni yule anayetimiza Masharti yafuatayo:

(1)Kuwa mtu anayeheshimu watu.
(2)Kuwa mtu anayefanya juhudi ya kuielewa, kuieleza, kuitetea na kuitekeleza Itikadi na Siasa ya CCM.
(3)Kuwa mtu mwenye kuamini kuwa kazi ni kipimo cha Utu, na kuitekeleza imani hiyo kwa vitendo.
(4)Kuwa mtu anayependa kushirikiana na wenzake

5)Kuwa mtu ambaye siku zote yuko mstari wa mbele katika utekelezaji wa mambo yote ya Umma, kulingana na Miongozo ya CCM.
(6)Kuwa wakati wote ni mfano wa tabia nzuri kwa vitendo vyake na kauli yake, kuwa mwaminifu na kutokuwa mlevi au mzururaji.
(7)Kuwa ama Mkulima, Mfanyakazi, au mwenye shughuli nyingine yoyote halali ya kujitegemea. Utaratibu wa kuomba Uanachama Utaratibu wa kufikiria maombi ya Uanachama Mafunzo kwa Wanachama Kiingilio na Ada za Uanachama
10. 9.Mtu atakayetaka kuwa Mwanachama atajaza fomu ya maombi na kuipeleka kwa Katibu wa Tawi anapoishi.

10.Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Tawi itafikiria na kutoa uamuzi wa mwisho kuhusu maombi ya Uanachama.
11.CCM itakuwa na Mpango wa kutoa Mafunzo kwa wanachama wake juu ya Imani, Malengo na Madhumuni ya Siasa ya CCM kwa jumla.
12.(1)Mtu akikubali kuwa Mwanachama itabidi atekeleze haya yafuatayo:

(a)Atatoa kiingilio cha Uanachama.
(b)Atalipa ada ya Uanachama kila mwezi isipokuwa kama akipenda anaweza kulipa ada ya mwaka mzima mara moja.
(c)Atatoa michango yoyote itakayoamuliwa.
(2) Viwango vya kiingilio, ada na michango vitawekwa na Halmashauri Kuu ya Taifa.

13.(1) Uanachama wa mwanachama utakwisha kwa:
(a)Kujiuzulu mwenyewe;
(b)Kuachishwa kwa mujibu wa Katiba. (c)Kufukuzwa kwa mujibu wa Katiba.
(d)Kutotimiza masharti ya uanachama.
(e)Kujiunga na Chama kingine chochote cha siasa.

(2)Mwanachama ambaye uanachama wake unakwisha kwa sababu yoyote ile hatarudishiwa kiingilio alichokitoa, ada aliyotoa wala michango yoyote aliyoitoa.
(3)Mwanachama aliyeachishwa au kufukuzwa Uanachama akitaka kuingia tena katika CCM, itabidi aombe upya, na atapeleka maombi yake hayo ama katika Halmashauri Kuu ya Wilaya ama kikao kilichomwachisha au kumfukuza Uanachama.
(4) Mwanachama aliyejiuzulu akitaka kuingia tena katika CCM ataomba upya kwa kufuata utaratibu wa kuomba Uanachama kwa mujibu wa Katiba ya CCM.

14.Mwanachama yeyote atakuwa na haki zifuatazo:-
(1)Haki ya kushiriki katika shughuli zote za CCM kwa kufuata utaratibu uliowekwa.

(2)Haki ya kuhudhuria na kutoa maoni yake katika mikutano ya CCM pale ambapo anahusika kwa mujibu wa Katiba.
(3)Haki ya kuomba kuchaguliwa kuwa Kiongozi wa CCM na ya kuchagua viongozi wake wa CCM kwa mujibu wa Katiba au Taratibu za CCM.
(4)Haki ya kujitetea au kutoa maelezo yake mbele ya Kikao cha CCM kinachohusika katika mashtaka yoyote yaliyotolewa juu yake, pamoja na haki ya kukata rufani ya kwenda katika Kikao cha juu zaidi cha CCM kama kipo endapo hakuridhika na hukumu iliyotolewa.

(5)Haki ya kumuona kiongozi yeyote wa CCM maadam awe amefuata utaratibu uliowekwa.
Wajibu wa Mwanachama
15.Kila Mwanachama atakuwa na wajibu ufuatao:

(1)Kujua kwamba Chama Cha Mapinduzi ndicho chenye nguvu, uwezo na kwamba nguvu hizo zinatokana na umoja wa Wanachama, fikira sahihi za CCM na kukubalika kwake na umma. Kwa hiyo kulinda na kuendeleza mambo hayo ni Wajibu wa kwanza wa kila Mwanachama.
(2)Kutumikia nchi yake na watu wake wote kwa kutekeleza wajibu wake bila hofu, chuki wala upendeleo wa nafsi yake, rafiki au jamaa.

(3)Kujitolea nafsi yake kuondosha Umasikini, Ujinga, Maradhi na Dhuluma, na kwa jumla kushirikiana na wenzake wote katika kujenga Nchi yetu.
(4)Kuwa wakati wote mkweli, mwaminifu na raia mwema wa Tanzania.
(5)Kukiri kwa imani na kutekeleza kwa vitendo Siasa ya CCM ya Ujamaa na Kujitegemea

6)Kujielimisha kwa kadiri ya uwezo wake, na kutumia elimu hiyo kwa faida ya wote.
(7)Kuwa tayari kujikosoa na kukosolewa ili kuweza kuwa na msimamo sahihi wa siasa ya CCM.
(8)Kuwa wakati wowote hadaiwi ada zozote za Uanachama.
(9) Kuhudhuria mikutano ya CCM inayomhusu

FUNGU LA II VIONGOZI
Maana ya Kiongozi Sifa za Kiongozi Miiko ya Kiongozi:
14. 16.Kiongozi wa CCM ni kila Mwanachama mwenye dhamana yoyote katika CCM aliyechaguliwa au kuteuliwa kwa mujibu wa Katiba.
17.Pamoja na kutimiza masharti ya Uanachama kama yalivyoelezwa katika Katiba, Kiongozi sharti pia awe na sifa zifuatazo:
(1)Awe ni mtu aliyetosheka na asiwe mtu aliyetawaliwa na tamaa.
(2)Awe ni mtu anayependa kueneza matunda ya Uhuru kwa wananchi wote kwa ajili ya manufaa yao na maendeleo ya Taifa kwa jumla.
18.Ni mwiko kwa kiongozi:-
(1)Kutumia madaraka aliyopewa ama kwa ajili ya manufaa yake binafsi au kwa upendeleo, au kwa namna yoyote ambayo ni kinyume cha lengo lililokusudiwa madaraka hayo.
(2)Kupokea mapato ya kificho, kutoa au kupokea rushwa, kushiriki katika mambo yoyote ya magendo au mambo mengine yaliyo kinyume cha lengo lililokusudiwa madaraka hayo
19. (1) Uongozi wa kiongozi utakoma kwa:
(a) Kujiuzulu mwenyewe.
(b)Kuachishwa kwa mujibu wa Katiba. (c) Kufukuzwa kwa mujibu wa Katiba.
(d)Kung’atuka /kuacha kazi.
(e) Kujiunga na chama kingine cho chote cha siasa.

(2)Kiongozi aliyeachishwa au kufukuzwa uongozi anaweza kuomba tena nafasi ya uongozi wowote na maombi yake yatafikiriwa na kutolewa uamuzi na kikao kilichomwachisha au kumfukuza uongozi.
20.(1) Mwanachama anayeomba nafasi ya uongozi wa aina yoyote katika CCM hatakubaliwa kuwa amechaguliwa mpaka awe amepata zaidi ya nusu ya kura halali zilizopigwa.
(2)Katika uchaguzi wa kujaza nafasi nyingi kwa pamoja, ushindi utahesabiwa kwa kufuata wingi wa kura alizopata mwombaji wa nafasi hiyo zaidi ya wenzake, bila kujali kama kura hizi zinafikia nusu ya kura zote
Mfano wa madudu katika katiba hiyo ni vifungu hivi hapa chini vinavyompa fursa "mhalifu" kuongoza chama/nchi.
13 (3)Mwanachama aliyeachishwa au kufukuzwa Uanachama akitaka kuingia tena katika CCM, itabidi aombe upya, na atapeleka maombi yake hayo ama katika Halmashauri Kuu ya Wilaya ama kikao kilichomwachisha au kumfukuza Uanachama.
(4) Mwanachama aliyejiuzulu akitaka kuingia tena katika CCM ataomba upya kwa kufuata utaratibu wa kuomba Uanachama kwa mujibu wa Katiba ya CCM.

19 (2)Kiongozi aliyeachishwa au kufukuzwa uongozi anaweza kuomba tena nafasi ya uongozi wowote na maombi yake yatafikiriwa na kutolewa uamuzi na kikao kilichomwachisha au kumfukuza uongozi.
Kinyume chake, vifungu hivihivi vinawafinya na kuwatosa wanafiki wa kisiasa, hili litatikea ikiwa wezi watatumia ukwasi walionao kuinunua kamati kuu ya ccm ili iwape ridhaa ya kugombea!
Hiyo ndio katiba ya chama mufilisi kinacholitafuna taifa usiku na mchana
"Kuna watu wasipokuelewa maneno na matendo yako, mshukuru Jah, wewe bado unafikra chanya, wakianza kukuelewa jichunguze ni wapi umeanguka maana umeanza kuwaza kama wao"

0 comments:

Chapisha Maoni