Shule ya Msingi Kibara B, iliyoko wilayani Bunda mkoani Mara,
imefungwa na wananchi kwa muda kutokana na watu wasiofahamika kujisaidia
kwenye vyumba vya madarasa, hali inayohatarisha afya za wanafunzi.
Mwenyikiti wa Kijiji cha Kibara B, Mafwili Mnyaga alisema kuwa shule hiyo imefungwa kwa muda usiojulikana tangu Aprili 28.
Alisema shule hiyo, iliyoko katika Mji Mdogo wa
Kibara, imefungwa na wananchi wa kijiji hicho baada ya walimu kukuta
asubuhi kila chumba kimejaa vinyesi milangoni, maeneo ya nje, pamoja na
vyooni.
Aidha, alisema kuwa mbali na hali hiyo, pia
mashimo ya vyoo hivyo yalikutwa yamezibwa kwa vitu vigumu, huku vinyesi
vingine vikiwa kwenye ndoo za maji zinazotumiwa na wanafunzi kwa ajili
ya kufanyia usafi.
Alisema kuwa, baada ya walimu wa shule hiyo ambayo
iko katikati ya makazi ya watu, kukuta hali hiyo kwenye kila darasa
walitoa taarifa kwa uongozi wa kijiji hicho ambao ulichukua hatua ya
kuifunga shule kwa muda.
Baada ya kufika shuleni hapo na kufanya mkutano, wananchi waliazimia kuwaruhusu watoto warudi nyumbani na kuifunga shule hiyo kwa mudaalisema.
Aliongeza kuwa walichukua hatua hiyo kwa kuhofia
watoto kuugua magonjwa yasiyofahamika kwani wanaofanya tukio hilo
hulifanya usiku na pia hawajui madhumuni yao.
Tayari uongozi wa kijiji umeandika barua kwenda
kwa mkurugenzi mtendaji wa wilaya na mkuu wa wilaya kuomba msaada na
ufumbuzi wa suala hilo.
Tumeifunga shule kwa sababu hali hii ni mbaya na tatizo hili halikuanza leo na linafanyika nyakati za usiku.
0 comments:
Chapisha Maoni