Ilikuwa ni safari ya kawaida ambayo ilitarajiwa kuwapa faraja
watoto. Lakini hali imekuwa tofauti baada ya matarajio hayo kugeuka
majonzi kwa mtaa mzima kutokana na kuondokewa na watoto watatu kwa
wakati mmoja.
Ni mara chache sana watoto hutoka pamoja kwenda
mbali kufurahia na wenzao. Hivyo Janet, Ndimbumi na Eva waliamini kuwa
siku hiyo ingewapa furaha na pengine hadithi za kwenda kusimulia
shuleni, lakini haikutokea kama walivyotarajia; simulizi zikawa tofauti.
Tulistuka kuuona mwili wa Janeth ukiwa unaelea juu ya majianasema kaka yake, Goodluck Kihoko (14) ambaye siku hiyo alienda pamoja na watoto wengine 20 kwenye Hoteli ya Landmark iliyo Mbezi Beach, jijini Dar es salaam.
Tuliwaita walinzi, lakini wakapuuza. Tuliwaita walinzi kwa muda mrefu ndipo wakafika na wakati huo mama na wale vijana walikuwa mbali na pale tulipokuwa tukiogelea. Baada ya muda walikuja na tukauona mwili wa pili ukiibukaanasimulia Gooluck kwa uchungu.
Wakisimulia tulio hilo, watoto waliokuwa katika
msafara huo Florian Masonda (12) anasema walichukuliwa na jirani yao,
Anita Mboka kwenda kusherehekea nao siku ya kuzaliwa kwa mtoto wake,
Derick Mboka aliyekuwa anatimiza umri wa mwaka mmoja.
Florian anasema baada ya kufika hotelini hapo
walianza kucheza mpira wa kikapu huku watoto wengine wakiogelea na mama
Mboka aliyewapeleka pamoja na wale vijana wakiwa wamekaa wakipata
vinywaji.
Tulikuwa tunacheza mpira wa kikapu na ghafla tulisikia kelele baada ya mtoto mmoja kuja kutuita na kutupatia taarifa kuwa kuna watoto wamezama chini ya maji na hawaonekani. Tuliondoka na baada ya kufika kwenye bwawa la kuogelea ndipo tulipowaona wakiwa tayari wamekunywa maji mengianasema Florian.
Naye Goodluck anasema yeye na watoto wenzake zaidi
ya 20 waliondoka Kijitonyama wakiwa na vijana wanne kwenda kwenye
sherehe hiyo.
Tuliondoka hapa saa kumi na moja jioni, baada ya kufika kule tulianza kuogelea kwenye bwawa. Watoto wengine walikuwa wanakwenda kuogelea kwenye maji marefu, walizuiliwa mara tatu, lakini baada ya walinzi kuondoka walirudi na kuzamaanasema.
Kwa uchungu alionao Bahati Sisala alikuwa amekaa
akiwa ameduwaa macho yake yamevimba na mekundu kutokana na machozi
yaliyomtoka kwa muda mrefu.
Akiwa amejiinamia bado haamini mkasa uliomkuta
binti yake kipenzi Ndimbumi Sisala (9) uliosababisha kifo chake ambacho
kilimkuta ghafla katika hoteli hiyo Aprili 27.
Lugano Mwakyosi, ambaye ni msemaji wa familia hiyo
inayoishi Kijitonyama Mpakani A, anasema Sisala amechanganyikiwa
kutokana na kifo cha binti yake aliyempenda sana.
Baba yake haamini kilichotokea mpaka sasa. Alikuwa anampenda sana binti yake licha ya kwamba alikuwa wa mwisho kuzaliwa kati ya watoto wake wanne, Ndimbumi alikuwa binti wa pekee na tegemeo kubwa katika familia yakeanasema Mwakyosi.
Anasema Sisala alihojiwa na polisi kabla ya safari
ya kwenda kuupumzisha mwili wa mwanaye mkoani Mbeya na kutoa tamko
kwamba hana kinyongo na jirani yake akiamini kwamba ulikuwa mpango wa
Mungu.
Baba mzazi wa marehemu amesema hana kinyongo na mzazi mwenzake kwani hakuwachukua watoto kwa nia mbaya, bali anaamini kwamba ni mpango wa Mungu japokuwa inamuuma sana kutokana na kufiwa na binti yake, aliyekuwa akisoma darasa la nne katika Shule ya Msingi Kijitonyamaanasema.
Sisala si mzazi pekee aliyefiwa katika mtaa huo.
Devotha Mbutwa ni mzazi mwingine aliyepoteza mtoto wake, Janeth Kihoko
(9) aliyekuwa akisoma Shule ya Msingi Dk. Omary Ali Juma darasa la nne.
Mbutwa anasema siku ya tukio watoto wake
walimpigia simu wakiomba ruhusa ya kwenda kwenye sherehe hiyo na baadaye
wangekwenda ufukweni.
Niliwakatalia, lakini wakanipigia tena na tena. Niliwaruhusu baada ya kuniambia kwamba wangekwenda hotelini tu bila kupita ufukweni. Kilichonishangaza baadaye nilipigiwa simu na kupewa taarifa za kifo cha binti yanguanasimulia kwa majonzi.
Mama huyo anasema hakukuwa na taarifa zozote
alizopewa na jirani yake kuhusu sherehe hiyo. Mwili wa Janeth
ulipumzishwa Jumatano katika Kijiji cha Viwengi, Wilaya ya Kilolo,
Iringa.
Akitoa ushuhuda wa tukio hilo, Nicholaus
Mwakatobe, baba mzazi wa marehemu Eva Mwakatobe (11), aliyekuwa akisoma
darasa la tatu katika Shule ya Msingi Shekilango, anasema:
Mpaka saa hii sijaona polisi wakinihoji wala kufika kumhoji yule mama, bado yupo hapa mtaani na aliwachukua watoto bila idhini ya wazazi.
Daria Andrew, bibi wa marehemu Eva, anasema mjukuu
wake aliaga anakwenda kwenye sherehe ya kuzaliwa, lakini hakutarajia
kama hayo yangetokea.
Alichukuliwa hapa kama anakwenda kwenye sherehe ya kuzaliwa huyo mtoto wa jirani yangu, aliniarifu wiki moja kabla wakati wa sherehe ya Pasaka, nilidhani ingekuwa salama japokuwa sikumruhusu kwenda kuingia katika majianasema Daria.
Hali ilivyokuwa mtaani
Vilio na simanzi vilitawala katika Mtaa wa
Kijitonyama Mpakani A kutokana na nyumba tatu za waumini waliokuwa
wakisali Jumuiya pamoja kuwa na msiba.
Hali hiyo iliwalazimu majirani kuzunguka kutoka nyumba moja
baada ya nyingine wakiwa na nia ya kuwapa moyo na kuwafariji wafiwa.
Kama unavyoona, tangu usiku wa jana tunazunguka nyumba moja baada ya nyingine. Tunakaa hapa kwa Mwakatobe kwa muda mfupi na baadaye tunaondoka na kwenda nyumba nyingine, hii yote ni katika kuwafariji wafiwa. Ni msiba mzito sana na haijawahi kutokea katika mtaa wetuanasema Jamila Husein mkazi wa Mpakani A.
Anita Mboka, mama anayedaiwa kuwachukua watoto hao
hakupatikana baada ya kujifungia nyumbani kwake na majirani walisema ni
kutokana na hofu ya msiba huo.
Alipopigiwa simu, ilipokelewa na mtu mwingine aliyesema kuwa mama huyo asingeweza kuzungumza kwa kuwa hali yake haikuwa nzuri.
Meneja wa Hoteli ya Landmark, Moshi Mbully anasema
vifo vya watoto hao ni ajali iliyotokea ghafla kwani mabwawa ya
kuogelea huwa na walinzi wawili mpaka watatu.
Tunasikitika sana kutokana na ajali hii. Tunafuatilia kwa ukaribu msiba huu na tayari tumeshakutana na familia zote tatu. Mbaya zaidi watoto walikatazwa zaidi ya mara tatu wasielekee eneo lenye maji mengi lakini kwa bahati mbaya walikaidianasema Mbully.
Kamishna wa polisi Kanda ya Dar es Salaam,
Suleiman Kova anasema baada ya watoto hao kuopolewa na kupelekwa
Hospitali ya IMTU iliyopo Mbezi walikuwa tayari wameshafariki dunia na
hivi sasa bado uchunguzi wa vifo hivyo unaendelea.
Kutokana na uangalizi hafifu katika hoteli
mbalimbali hapa nchini, Kamanda Kova anasema jeshi lake kwa sasa
limejipanga kufuatilia kila hoteli ili kubaini kama ina wasimamizi wa
mabwawa hayo ili kuokoa maisha ya watu.
Tukio hili linanisikitisha sana hasa ukizingatia
hawa ni watoto wa taifa la kesho, na hii inaonyesha kuwa mabwawa mengi
ya kuogelea hayana wasimamizi hivyo kuwa rahisi kwa watoto kuingia na
kuogelea. Kungekuwa na wasimamizi vifo vya watoto hao visingetokea.
Kutokana na uzembe huu jeshi langu litafanya utaratibu wa kukagua kila
hoteli yenye bwawa la kuogelea kuhakikisha linakuwa na msimamizi,”
anasema Kova. Sheria za umiliki wa mabwawa ya kuogelea inataka kuwepo
kwa walinzi wakati wote, na hii ni katika mabwawa ya wakubwa na yale ya
watoto.
Ajali za aina hii zimekuwa zikitokea mara kwa mara
hali inayoashiria kuwa miongozo hii haifuatwi. Ili kupunguza ajali na
kuokoa maisha ya watu, ni lazima wasimamizi wa miongozo hii watimize
wajibu wao.
0 comments:
Chapisha Maoni