Wanafunzi wapatao tisa wamefariki dunia wakati wa maandamano ya siku kadha katika jimbo la Oromia nchini Nigeria.
Hata hivyo, mtu aliyeshuhudia tukio hilo ameiambia BBC kuwa watu 47 waliuawa na majeshi ya usalama.
Amesema maandamano ya Ambo, kilomita
125 magharibi mwa mji mkuu Addis Ababa yalianza Ijumaa wakipinga
mipango ya kupanua mji mkuu huo hadi katika maeneo ya jimbo la Oromia.
Serikali haijasema namna vingi vya vifo hivyo
vilivyotokea lakini mkaazi huyo wa Ambo anasema aliona wanajeshi
wakifyatua risasi za moto.
Niliona zaidi ya miili 20 mitaani
amesema.
Najificha ndani ya nyumba yangu kwa sababu naogopa.
Mkaazi huyo wa Ambo amesema wanafunzi wanne
waliuawa Jumatatu na wengine 43 waliuawa katika msako mkali Jumanne,
baada ya maandamano makubwa yaliyohusisha pia watu wasio wanafunzi.
Tangu wakati huo, mitaa ya mji huo imekimbiwa, amesema, benki na maduka vimefungwa na hakuna usafiri.
Amesema shughuli za ufundishaji zimesitishwa
katika chuo kikuu cha Ambo, ambako maandamano yalianzia, na wanafunzi
walizuiwa kuondoka.
Katika taarifa yake serikali ya Ethiopia imesema
watu wanane walipoteza maisha wakati wa ghasia za maandamano hayo
yaliyoongozwa na "majeshi ya kupinga amani" katika miji ya Ambo na
Tokeekutayu, na katika chuo kikuu cha Meda Welabu, ambacho pia kiko
katika jimbo la Oromia.
0 comments:
Chapisha Maoni