Hatimaye beki wa kulia wa Arsenal, Bacary Sagna amekamilisha usajili wake Manchester City kwa kupewa mkataba wa miaka mitatu.
Sagna amemaliza mkataba wake Arsenal, ambapo wakuu wa Emirates
walikuwa wakivuta miguu kumpatia mkataba mpya kwa sababu ya umri wake.
Sagna (31) alikuwa kichocheo kikubwa cha mafanikio Arsenal msimu
uliomalizika majuzi lakini Arsenal waliona kwamba umri na fedha
alizokuwa akidai vilikuwa juu.
Inaelezwa kwamba awali alipewa mkataba wa mwaka mmoja Arsenal
akakataa, akapewa wa miaka miwili lakini wakashindwana kwenye malipo,
akaamua kuondoka.
Alicheza mechi yake ya mwisho kwenye fainali ya Kombe la Ligi
wikiendi iliyopita ambapo Arsenal waliibuka na taji baada ya miaka tisa.
Inaelezwa kwamba mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England wamempa mkataba ambao atalipwa pauni 150,000 kwa wiki, ikiwa ni nyongeza kubwa kutoka pauni 80,000 alizokuwa akilipwa Arsenal.
Inaelezwa kwamba mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England wamempa mkataba ambao atalipwa pauni 150,000 kwa wiki, ikiwa ni nyongeza kubwa kutoka pauni 80,000 alizokuwa akilipwa Arsenal.
Hata hivyo, Sagna ambaye kocha Arsene Wenger alijaribu kumbakiza,
alikuwa akitaka nyongeza hadi pauni 200,000 na miaka mitatu zaidi hapo
Emirates, kiwango ambacho kikilinganishwa na umri wake waliona hakikidhi
mahitaji.
Sagna alikuwa pia akitakiwa kusajiliwa na klabu nyingine kubwa Ulaya
kama Paris Saint Germain, na Monaco za Ufaransa na Galatasaray ya
Uturuki.
Kutokana na mazingira hayo, Arsenal wameshaanza mazungumzo kwa ajili
ya kumsajili Serge Aurier anayecheza Toulouse ya Ufaransa kuziba nafasi
ya Sagna.
Aurier anayethaminishwa kwa pauni milioni saba amesema wazi kwamba
hawezi kukataa ofa kutoka klabu yoyote ya Ligi Kuu England, hata
zilizopanda daraja msimu huu kwa sababu ni ligi kubwa.
Arsenal wameshaanza mazungumzo na klabu yake, ambapo watalazimika
kutoa fungu huku Sagna, akiondoka na kusajiliwa bure huko aendako kwa
kuwa ni mchezaji huru.
0 comments:
Chapisha Maoni