Alhamisi, Mei 22, 2014

MCHUMBA WA ADAM KUAMBIANA AIBUKA

Siku mbili tu baada ya mazishi ya mwigizaji na mwongoza filamu mahiri Bongo, marehemu Adam Kuambiana, mrembo mmoja ameibuka na kusema alikuwa mchumba wa marehemu

Kwa mujibu wa mrembo huyo, Lulu Jumanne ‘Selina’, alifahamiana na marehemu Kuambiana mwaka 2006 akamwambia ndoa yake haipo sawasawa.
Alisema walianzisha uhusiano lakini haukuwa wazi katika jamii. Alisema siku moja akiwa anaishi Mwananyamala, wazazi wake walimtembelea.
Nikiwa na wazazi nilimwona Kuambiana anapiga hodi, akaingia akiwa na  begi la nguo. Niliogopa kwani wazazi walikuwepo na walikuwa hawamtambui.
Hata hivyo, walielewa yakapita, tukawa tunaishi wote nyumbani kwa kupika na kupakua
 alisema Selina ambaye naye ni mwigizaji.
Aliendelea kuweka wazi kwamba, baada ya hapo maisha yaliendelea lakini ikafika mahali marehemu akahamishia mapenzi kwa Mbongo Fleva, Stara Thomas yeye akawa ‘zilipendwa’.
Akizidi kuanika mambo kuwa mwaka jana Kuambiana alirudi kwake baada ya kutofautiana na Stara, akataka waendelee na mapenzi yao.

0 comments:

Chapisha Maoni