Ijumaa, Mei 09, 2014

NUSURA DIDA ASAGWE UKUMBINI MANGO GARDEN

Mtangazaji wa Radio Times FM, Hadija Shaibu ‘Dida’ amezua timbwili baada ya kung’ang’aniwa na mwanamke mwenzake aliyedaiwa kutaka kumshawishi afanye naye mapenzi ya jinsi moja (usagaji).
Dida alikumbwa na ishu hiyo, Alhamisi ya wiki iliyopita ndani ya Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni jijini Dar, wakati Kundi la Mashauzi Classic, lilikuwa likiangusha burudani.
Katika tukio hilo lililoshuhudiwa na chanzo chetu, mwanamke huyo aliyetajwa kwa jina moja la Addy ambaye anadaiwa kukubuhu kwa tabia hiyo chafu ya usagaji.
Ilisemekana kwamba mwanadada huyo alianza kumzengea Dida kwa kumsemesha huku akimuonesha pozi za kimahaba.
Pamoja na Dida kumpuuza, Addy alifika mbali na kuanza kumshtua kwa kutokea nyuma yake kwa kumtekenya huku akimkonyeza na kumshawishi waongee vizuri.
Kutokana na vitendo hivyo, Dida alipandwa na hasira na kuchukua chupa kutaka kumpasua ndipo Addy naye akawa anahangaika kujitetea na kusababisha vurugu katika eneo hilo, shukrani ziwaendee wasamaria wema waliwatuliza.
Dida alisema:
Huyu dada ni muda mrefu alikuwa akinisumbua hapa ukumbini, mwanzo nilikuwa sijajua anachotaka kumbe ni mshenzi kabisa, anataka kunifanya vitendo vya kisagaji, amenikera sana.

0 comments:

Chapisha Maoni