Staa wa sinema za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amejikuta kwenye wakati
mgumu baada ya kutukanwa matusi ya nguoni na mwanadada anayejulikana
kwa jina la Muna Alphonce kisa, kikidaiwa ni mwanaume.
Habari ya mjini ilieleza kwamba Muna ambaye ni mke wa mtu
aliporomosha matusi ya nguoni ambayo siwezi kuyaandika hapa mtandaoni huku akimtoa
kasoro mbalimbali Nisha na kumweleza kuwa hakuwahi kufikiria wala kuwa
na uhusiano wa kimapenzi na mpenzi wake wa sasa kwani ana mume na
familia.
Sina uhusiano na mwanaume wa Nisha ila kuna siku moja alinipigia simu na kujitambulisha kwangu kwamba anahitaji tufanye biashara kwani anafanya biashara ya magari lakini nikampotezea, akarudia tena mara ya pili pia nikampotezea lakini sasa nashangaa Nisha kudai ninamtaka mwanaume wake. Wewe nisha nikome kabisa
alisema Muna.
Baada ya kuzinyaka habari hizo na matusi hayo ya nguoni, Baada ya Nisha kuulizwa kuhusiana na hilo, amejibu kwa kuyasema haya:
Mimi sigombei mwanaume na mtu. Mwanaume wangu ninampenda na yeye ananipenda japokuwa watu wanazungumza mengi
alisema Nisha.
0 comments:
Chapisha Maoni