Jumapili, Mei 25, 2014

SABABU KUBWA TATU ZA NDOA YA VICKY KAMATA KUYEYUKA

Hadi taarifa zinafika mtandaoni katika Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mkombozi, Sinza jijini Dar juzi saa 10:00 jioni, ndoa ya Mbunge Vicky Kamata iliyokuwa ifungwe hapo iliyeyuka.
Vicky Kamata ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum kwa tiketi ya UVCCM, Mkoa wa Geita alikuwa afunge ndoa na mwanaume aliyejulikana kwa jina la Charles wa jijini Dar.
Vicky Kamata akiwa amelazwa baada ya kuugua ghafla katika Hospitali ya Tabata General jijini Dar.
Baada ya kuona muda unakwenda bila kuwepo kwa dalili za wahusika kufika  kufunga ndoa hiyo ambayo harusi yake ilidaiwa ingetumia shilingi milioni 96, wanahabari wetu walimtafuta Baba Paroko, Cuthbert Maganga ili kumsikia anasema nini kuhusu hilo.
Hata hivyo, mtu aliyedai ni katekista wa kanisa hilo alisema paroko alikwenda hija, Buguruni, Dar.
Kuhusu ndoa ya Vicky Kamata, katekista huyo alidai Jumapili ya Mei 18, 2014 ndani ya ibada za kanisa hilo ilitangazwa hadharani ‘laivu’ kwamba haitafungwa. 
Vicky na Charles wakila bata.
SABABU YA KWANZA
Kwa mujibu wa chanzo, mwanaume aliyetaka kufunga ndoa na Vicky ana ndoa nyingine ya kanisa na imejaliwa kupata watoto kadhaa hivyo isingekuwa rahisi kufungwa kwa ndoa nyingine kwa mujibu wa maandiko ya Biblia. Mume mmoja mke mmoja mpaka kifo kiwatenganishe.

SABABU YA PILI
Sababu ya pili ilielezwa kuwa, Vicky asingeweza kufunga ndoa hiyo kwani mwanaume huyo alishatoa mahari kwa msichana mmoja (jina tunalo) wa jijini Dar na ukweni anajulikana.
Alishatoa mahari kwa msichana mwingine mbali na Vicky, ukweni anajulikana.
Sasa ilipotoka ile picha yake kwa mara ya kwanza kwenye Gezeti la Ijumaa (Mei 16, 2014) yenye kichwa cha habari ndoa ya Vicky itatumia shilingi milioni 96 ikawa kasheshe kwa yule msichana na ukweni, ndiyo jamaa akaamua kutangaza kubatilisha ndoa na Vicky
kilisema chanzo.

SABABU YA TATU
Sababu ya tatu ilitajwa ni kitendo cha kuumwa. Wikiendi iliyopita, Vicky aliugua ghafla na kulazwa katika Hospitali ya Tabata General jijini Dar kwa hiyo isingekuwa rahisi ndoa kufungwa Jumamosi kutokana na hali yake kuwa mbaya.

0 comments:

Chapisha Maoni