Mahakama nchini Sudan imemhukumu kifo mwanamke mmoja anayedaiwa kubadili dini yake na kuolewa na mwanamume mkristo.
Daktari Mariam Yahya Ibrahim Ishag, ambaye
babake ni muisilamu alishitakiwa kwa kosa la kuasi dini pamoja na
kufanya zinaa kwa kuolewa na mwanamume mkristo , kitu ambacho dini ya
kiisilamu imeharamisha kwa wanawake.
Mariam mwenye umri wa miaka 27 pia
ni mjamzito na pia atapata adhabu ya mijeledi miamoja kwa kosa la zinaa.
Maafisa wakuu wanasema kuwa icha ya Mariam kulelewa kwa njia ya
kikristo yeye bado ni muisilamu kwa sababu hiyo ndiyo dini ya babake.
Kwa kawaida wanawake waisilamu hawaruhusiwi
kuolewa na wanaume wakristo ingawa wanaume waisilamu wanaruhusiwa kuwaoa
wanawake wakristo.
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu
Amnesty International linasema kuwa Bi Ishag alilelewa kama Mkristo
muorthodoxi kwa sababu babake hakuwepo naye maishani mwake.
0 comments:
Chapisha Maoni