Mwanamke aliyeasi dini nchini Sudan na kupata adhabu
ya kifo amejifungua mtoto mvulana akiwa jela mjini Khartoum kwa mujibu
wa wakili wake.
Meriam Yehya Ibrahim Ishag, aliolewa na
mwanamume mkristo jambo lililopelekea mwanamke huyo kuhukumiwa kifo
mapema mwezi huu baada ya kukataa kusilimu tena.
Ataruhusiwa kumnyonyesha mtoto wake kwa miaka miwili kabla ya hukumu kutekelezwa.
Meriam aliyezaliwa na wazazi waisilamu, alihukumiwa na mahakama ya ya kiisilamu.
'Mijeledi miamoja'
Bi Ibrahim alihukumiwa kifo kwa kosa la zinaa
kwa sababu ameolewa na mwanamume mkristo wa kutoka Sudan Kusini na
kwamba ndoa yao haikubaliki chini ya sheria ya kiisilamu ambayo inasema
kuwa mwanamke musilamu hawezi kuolewa na mwanamume mkristo.
Kwa kosa hilo, jaji alimuhukumu adhabu ya
mijeledi miamoja, adhabub ambayo itatelezwa pindi mama huyo atakapopata
nafuu kutokana na kujifungua.
Bi Ibrahim alilelewa kwa njia ya kikristo , dini
ya mamake kwa sababu babake aliyekuwa muisilamu hakuwepo katika maisha
yake tangu utotoni.
Kwa mujibu wa shirika la kimataifa la Amnesty
International, alikamatwa na kushitakiwa kwa kosa la Zinaa mwezi Agosti
mwaka 2013, na mahakama ikamuongezea kosa la kuasi dini Februari 2014
aliposema kuwa yeye ni mkristo wala sio muisilamu.
Sudan ina idadi kubwa ya waisilamu ambao wanafuata sheria za kiisilamu.
0 comments:
Chapisha Maoni