Watu watatu wamefariki Mkoani Iringa kwa matukio matatu tofauti likiwepo la mtu mmoja kufariki kwa kujinyonga baada ya kujua ameathirika ugonjwa wa Ukimwi.
Akithibitisha kutokea kwa matukio hayo Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani Iringa ACP Ramadhani Mungi amesema Msagala Kalenga mwenye umri wa miaka 25 Mkazi wa Kijiji cha Mapogoro Wilaya ya Iringa Vijijini Mkoani Iringa amekutwa amefariki kwa kujinyonga kwa kutumia mtandio.
Kamanda Mungi ameongeza kuwa jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi zaidi wa tukio hilo ambapo mwili wa marehemu ulikutwa jirani na mti uliokatwa pembeni ya mto Kalenga.
Aidha amesema mtoto Christiani Kipeto mwenye miaka 2 mkazi wa eneo la Mlandege Manispaa ya Iringa amefariki baada ya kuungua mguu kwa moto upande wa kushoto ulio sababishwa na mshumaa kuunguuza mito ya makochi.
Wakati huo huo Kamanda Mungi amesema Mtoto Lemiana Ndazi mwenye umri wa miaka 5 mkazi wa kijiji cha Magubike Wilaya ya Iringa Vijijini amekutwa amefariki kwenye korongo na mwili wake ukiwa umefungwa kwa sweta usoni na mtu/watu wasiofahamika.
Pia amesema chanzo cha tukio hilo bado kinachunguzwa zaidi ikiwa ni pamoja na jeshi la polisi Mkoani Iringa linaendelea kuwatafuta mtu/watu walio husika na mauaji ya mtoto.
Hata hivyo Kamanda Mungi amesema askari polisi wakiwa doria maeneo ya Ipogoro Manispaa ya Iringa wamewakamata Getachwe Nguruna mwenye umri wa miaka 15 na Takle Tapesa mwenye umri wa miaka 26 wote raia wa kutoka nchi ya Sudani wakiwa wameingia nchini bila kibali.

0 comments:
Chapisha Maoni