Kampuni kubwa duniani ya vifaa vye elektroniki,
Samsung inasema kuwa itawalipa fidia wafanyakazi wake waliougua Saratani
kutokana na kufanya kazi katika viwanda vyake.
Kampuni hiyo iliomba radhi kwa kesi ya muda
mrefu kati yake na wafanyakazi hao waliokuwa wanadai fidia na badala
yake kukubali kujiondoa katika kesi hiyo huku ikikubali kuwalipa fidia
wagonjwa hao.
Hatua ya Samsung kukubali kuwalipa
wafanyakazi hao inaleta matumaini katika kukamilika kwa mvutano huo
ambao ulionekana kukwama kwa muda mrefu
Lakini afisa mkuu mtendaji wa kampuni hiyo, Kwon
Oh-hyun nusura kukiri kuwa kulikuwa sababu ya wafanyakazi hao kupatwa
na Saratni ilichangiwa na wao kufanya kazi katika kiwanda cha Samsung.
Wengi walipata Saratani ya damu au Leukaemia.
Bwana Kwon alisema wafanyakazi kadhaa katika
viwanda vyetu walipatwa na Saratani ya damu na kuugua magonjwa mengine
yasiyokuwa na tiba ambayo yalisababisha baadhi yao kufariki.''
tulipaswa kumaliza kesi hii kitambo sana na bila shaka tunahisi uchungu kwamba tulikosa kufanya hivyo, tunaomba radhi kwa hilo
Akiongea na wandishi wa habari, Bwana Kwon
alisema kuwa Samsung inatumai kuwa itaweza kumaliza kesi hii na kuweza
pia kuwapa afueni wagonjwa na familia zao.
Hata hivyo kampuni hiyo kubwa zaidi duniani ya
simu za Smartphone haikusema idadi ya watu watakaolipwa fidia ingawa
inaarifiwa ni watu 40 waliowasilisha malalamiko hayo huku kesi
ikiendelea kwa zaidi ya miaka sita.
0 comments:
Chapisha Maoni