Jumatano, Mei 14, 2014

HUU NDIO MPIRA UTAKAOTUMIKA KATIKA FIFA 2014 BRAZIL

Je kifaa hiki kitaweza? Hilo ndilo swali linaloulizwa na wengi kuhusu Brazuca, jina la mpira rasmi utakaotumiwa katika dimba la Kombe la Dunia lijulikanalo kama Brazil 2014.
Mpira huo ni wa 12 kuundwa na kampuni ya Adidas kwa kinyang'anyiro cha Kombe la Dunia.

Kampuni hiyo ilikosolewa miaka minne iliyopita juu ya mpira uliojulikana kama Jabulani, mpira rasmi wa Kombe la Dunia wa mwaka 2010 Afrika Kusini.
hauna mwelekeo angani na hautabiriki
ndivyo alivyosema mlinda lango wa Italia Gianluigi Buffon, naye mshambulizi wa Brazil Luis Fabiano alisema mpira huo ulikuwa wa "kimiujiza".
Adidas sasa inadai kuwa Brazuca imeimarisha mguzo wake na shabaha.
Tumefanya uchunguzi unaohusiana na mwendo wa mpira huu na matokeo yanaonyesha kuwa unasafiri na kupaa kwa njia zinazotarajiwa na kujipinda kokote ni kudogo sana hivi kwamba hakutambuliki
mkurugenzi wa kandanda wa Adidas Matthias Mecking aliambia BBC.
Wataalamu wa kasi angani waliohojiwa na BBC walisema kuwa kuna sababu tatu zitakazotumiwa kuamua matumizi ya mpira wa Kombea la Dunia la Brazil 2014.

0 comments:

Chapisha Maoni