Wabunge kutoka eneo linalokuza mmea wa Khat au Miraa
la Meru mashariki ya Kenya wametishia kuwasilisha mswada bungeni
kulazimisha serikali kuwafukuza wakulima waingereza wanaoishi katika
eneo hilo.
Hii ni baada ya bunge la juu nchini Uingereza
kupiga kura na kuidhinisha sheria inayoweka marufuku ya kuingizwa mmea
huo nchini humo kutoka Kenya.
Waziri wa mambo ya ndani nchini
Uingereza, Theresa May amekuwa akipigia debe marufuku hiyo akisema kuwa
Miraa ni mmea unaolewesha kama dawa zingine za kulevya.
Wabunge hao wanasema kuwa wamejaribu mbinu zote
za kisheria na kidiplomasia kushawishi Uingereza kutoharamisha Miraa
kutoka Kenya ingawa wamekosa kufaulu.
'Itawakosesha ajira'
Wakulima wa Meru hukuza sana Miraa kama kilimo cha kuwapa mapato
Kadhalika Wabunge hao wanasema kuwa hatua ya kupigwa marufuku mmea huo itasababisha karibu watu milioni mbili kukosa ajira.
Mapema wiki hii bunge la malodi nchini Uingereza
liliidhinisha marufuku dhidi ya Miraa mapema wiki hii huku waziri wa
maswal ya ndani akionya kuwa kukosa kuharamisha Miraa ambayo inasemekana
kuwa katika kiwango sawa cha madawa ya kulevya m uingereza itageuka
kuwa eneo la kufantyia biashara haramu ya mmema huo.
Miraa hutumiwa sana na jamii za watu wa Yemen na wasomali nchini Uingereza.
Marufuku hiyo ndio chanzo cha hasira miongoni
mwa wakulima wa Kenya wanaokuza mmea huo ambao wabunge wao wanaitaka
serikali ya Kenya kuwafukuza wakulima waingereza wanaomiliki mashamba
katika eneo hilo.
Wanasema kuwa mashamba yao hutumiwa kukuza Miraa
na hayawezi kutumiwa kuapnda chakula kingine. Pia wabunge hao wanasema
kama marufuku hiyo ipo kweli basi wakulima wapewe mashamba mengine ya
kupanda chakula.
Wakulima waingereza wanamiliki karibu robo ya mashamba katika eneo la Meru wakipanda wimbi.
0 comments:
Chapisha Maoni