"Wananchi wanataka MABADILIKO ya Muundo wa Muungano na uendeshaji wake. Wananchi wanataka kusikilizwa Juu ya Muungano, hivyo njia pekee ni kuitisha KURA ya maoni.
Na kama Jibu lao litakuwa ni ndiyo, basi Wananchi waamue kupitia Kura hiyo ni Muundo gani wa Muungano wanautaka. Miaka hamsini (50years) ya Watawala kuamua masuala haya muhimu peke yao Inatosha". Kama hali hiyo Ilivyokuwa katika Bunge maalumu la Katiba, licha ya Bunge hilo kujazwa Wajumbe wengi wa CCM kutoka kundi la 201, hali ni mbaya zaidi nje ya Bunge hilo na nje ya Bunge lako tukufu. Nje ya Mabunge haya, Watu wengi hasa Wazanzibar ambao ndio wamekuwa waathirika wakubwa wa Muungano huu katika nusu Karne ya maisha yake, hawataki kuendelea na Muungano huu"
0 comments:
Chapisha Maoni