Mtanzania amekamwata katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta
Nairobi Kenya akiwa amebeba dawa za kulevya akiwa njiani kuelekea
Antananarivo ambapo mzigo huo ulitokea Tanga kisha ukapita Mombasa na
baadae kwa ndege mpaka Nairobi.
Mzigo wenyewe ni wa cocaine na Heroin ambazo zote zina thamani ya
zaidi ya shilingi milioni 24 za Kitanzania na dawa hizo alikua
ameziingiza katika njia ya haja kubwa.
Mkuu wa kitengo cha CID katika uwanja huo Joseph Ngisa amesema
mshukiwa alikamatwa JKIA na akawekwa kwenye chumba cha uchunguzi na
baadae akatoa tembe za cocain na tembe za Heroin na tayari ameshapelekwa
Mahakamani.
Mwezi March mwaka huu watanzania wanne walikamatwa katika uwanja
huohuo walipopatikana na heroin yenye thamani ya zaidi ya shilingi
milioni 75 za Kitanzania na wote walifikishwa mahakamani na kukiri kosa.
Wanawake watatu na mwanaume mmoja kila mmoja akishtakiwa kando kwa
kosa la kusafirisha dawa za kulevya na walikua wameingia Kenya kupitia
Namanga na walikamtwa wakiwa njiani kuelekea Hong Kong.
Kuanzia March 2014 mpaka leo hii May ni jumla ya Watanzania watano
wamekamatwa kwenye kiwanja cha ndege Nairobi wakiwa kwenye pilika za
kusafirisha dawa za kulevya kwenda kwenye mataifa mengine.




0 comments:
Chapisha Maoni