Ijumaa, Mei 16, 2014

MIKONONI MWA POLISI BAADA YA KUKUTWA NA KETE ZA BANGI

Jeshi la polisi linamshikilia mtu mmoja Aswile Andongwisye [24] mkazi wa Nkuyu wilaya ya Kyela kwa kukutwa bhangi kete 64 zenye uzito wa gram 320.
Tukio hilo limetokea tarehe jana majira ya saa nane na nusu mchana huko katika eneo la Nkuyu, kata ya Nkuyu, tarafa ya Unyakyusa, wilaya ya Kyela,mkoa wa Mbeya. Taratibu za kisheria zinafanywa ili mtuhumiwa ambaye ni mtumiaji na muuzaji wa bhangi afikishwe mahakamani.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed  Msangi anatoa wito kwa jamii kuacha kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya kwani ni kinyume cha sheria.

0 comments:

Chapisha Maoni