Ijumaa, Mei 16, 2014

WATU WATANO WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MBEYA KWA KUPIGA RAMLI YA KIUCHONGANISHI

Jeshi la polisi mkoa wa Mbeya linawashikilia watu watano [05] kutokana na misako mbalimbali iliyofanyika. Katika tukio la kwanza jeshi la polisi linawashikilia watu wanne kwa kosa la kupiga ramli chonganishi. Tukio hilo limetokea tarehe jana majira ya saa nane mchana huko katika kijiji cha Isangawana, kata ya Matwiga, tarafa ya kipembawe, wilaya ya chunya, mkoa wa Mbeya.
Watuhumiwa waliokamatwa ni 1. Tonny Ernest Kalamata [32], mkazi wa mkoani Tabora 2. Shaban Rashid [31], mkazi wa mkoani Tabora 3. Bailos ismail [31] mkazi wa dsm pamoja na mwenyeji wao emanuel Kabuka [30],mwenyekiti wa kijiji hicho ambaye pia ndiye aliyewaleta. Taratibu za kisheria zinafanywa ili wafikishwe mahakamani.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Msangi anatoa wito kwa jamii kuepuka na kuacha tabia ya kusadiki imani potofu za kishirikina kwani zina madhara makubwa ikiwa ni pamoja na kusababisha matukio ya mauaji na kurudisha nyuma maendeleo katika jamii. Na yeyote atayebaianika kufanya vitendo hivi polisi haitasita kuwakamata na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

0 comments:

Chapisha Maoni