Mchungaji Langeni Mwasibira (39) wa Kanisa la Baptist, lililopo Kyela
mkoani Mbeya yupo hoi hospitalini Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Mchungaji huyo yupo katika mateso makubwa baada ya gonjwa la ajabu
kumkumba na kuwapa hofu waumini wake, ambao hata baada ya kufunga kwa
ajili ya maombi, hali yake inazidi kuwa mbaya siku hadi siku.
Mwasibira, mkazi wa Kijiji cha Kisyosyo Kata ya Matema yupo
Muhimbili, Jengo la Sewahaji, wodi namba 23 akijiuguza baada ya kulazwa
katika hospitali mbalimbali nchini bila mafanikio.
Akisimulia kwa uchungu kisa cha ugonjwa wake huo, alisema ulimuanza
mwaka 1994, tena ukiwa kama kijidoa cheusi kabla ya kugeuka kipele
ambacho alipokwenda hospitali ya wilaya yao ya Kyela kwa ajili ya
kupimwa na kutibiwa, madaktari walishindwa kugundua tatizo na kumshauri
kwenda Hospitali ya Rufaa ya Mbeya.
Hiyo ilikuwa imeshachukua miaka minne sasa, hivyo mwaka 1998 nikaenda Mbeya, lakini nako walishindwa kuniambia tatizo langu hasa lilikuwa ni nini, uvimbe, muwasho na maumivu makali yalikuwa yanaongezeka, ikawalazimu kunifanyia upasuaji, lakini hakukuwa na unafuu zaidi ya uvimbe kuzidi kuumuka na maumivu kuongezeka
alisema.
Nikawa sipati usingizi kutokana na maumivu, mwaka 2000 nilifunga
safari ya kuja Muhimbili, nao walinipeleka hospitali ya magonjwa ya
kansa Ocean Road, nilipimwa lakini haikua kansa, nilirudishwa tena
Muhimbili, walinipima kwa mara nyingine wakagundua kuwa ni ugonjwa wa
neurofibroma, walidai wakiupasua utaumuka zaidi hivyo nirudi nyumbani.
Nililazimika kurudi nyumbani Mbeya, hata hivyo hali ilizidi kuwa mbaya, wakati mmoja nikasikia Kigoma kuna daktari bingwa wa magonjwa haya, nikalazimika kufunga safari, nako walifanya upasuaji, matokea yakawa mabaya zaidi, ulizidi kuvimba kiasi cha kukaribia kufunika jicho.
Nikiwa huko niliishiwa fedha, nililazimika kupiga simu nyumbani ambako walifanya mchango wa hela kwa ajili ya nauli yangu nirudi nyumbani, hata hivyo hali ilikuwa mbaya, nikaona bora nije tena hapa Muhimbili Aprili 21, mwaka huu.
Alisema anawashukuru madaktari kwani walimpokea kwa upendo na
kumchukua vipimo kwa mara nyingine, ambavyo hata hivyo, bado havijatoka.
Wakati yeye akiwa hoi kitandani Muhimbili, maumivu mengine
yaliongezeka hivi karibuni, baada ya kupokea simu kutoka kwa ndugu zake,
ikimfahamisha kuhusu kusimamishwa shule kwa watoto na mdogo wake ambao
alikuwa akiwasomesha kutokana na kutolipwa kwa karo wshilingi laki tisa.
Nina mke na watoto watano, kwa sasa mke wangu ndiye anahangaika nao
alisema.
0 comments:
Chapisha Maoni