KIFO cha ghafla cha mwigizaji na mwongoza filamu za
Kibongo, Adam Philip Kuambiana kimeibua mazito ya kutosha, Uwazi
limeshika kitu mkononi.
Moja kati ya mazito hayo ni kuwepo kwa madai kwamba marehemu alikula au alilishwa sumu kupitia chakula.
Moja kati ya mazito hayo ni kuwepo kwa madai kwamba marehemu alikula au alilishwa sumu kupitia chakula.
Kwa mujibu wa rafiki mmoja wa karibu wa Kuambiana aliyeomba hifadhi
ya jina lake, marehemu Kuambiana asingekufa ghafla kama tatizo lilikuwa
vidonda vya tumbo au kisukari, ila kuna sumu iliingia tumboni mwake
kupitia chakula.
Siku ile Kuambiana alikuwa ana pesa, alianza kunywa pombe kuanzia asubuhi lakini pia alikuwa anakulakula kila alipojisikia. Naamini katika kulakula huko ndiko alikumbana na janga hilo
alisema rafiki huyo.
Mtu huyo wa karibu alikwenda mbele
zaidi kwa kudai kwamba ana wasiwasi na baa moja ambayo hakuitaja kwa
jina kwamba huenda marehemu alikula hapo kwani alikuwepo kwa muda mrefu
siku ya Ijumaa.
Unajua ninaposema alikula chakula chenye sumu sina maana wahudumu walimwekea sumu kwa makusudi. Ila siku hizi kuna ‘food poison’ (sumu kwenye chakula) ambayo mtu anaweza kujikuta anakula kupitia chakula, soda au juisi bila kujijua,
alisema mtu huyo.
Wakati rafiki wa
karibu wa Kuambiana akiwa na wasiwasi na sumu, Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ambaye
alisema habari zilizoenea ambazo yeye amezisikia ni kuwa marehemu
alikunywa dawa (hakusema dawa gani) pia akanywa bia jambo ambalo kama ni
kweli alitengeneza sumu mwilini.
Binadamu wanasema mengi lakini mimi nilichosikia marehemu alikunywa
dawa halafu akanywa bia zake na ndiyo chanzo cha kifo chake cha ghafla.
Lakini mimi ninachoamini yule bwana amekufa kwa sababu ya vidonda vya tumbo (ulcers). Lakini pia alikuwa akisumbuliwa na kisukari (diabetes).
Unajua alipewa masharti asinywe pombe halafu msosi uwe wa uhakika sasa inaonekana kwenye kuyazingatia hayo masharti ndiyo ikawa shida kidogo
alisema Steve Nyerere.
Nje ya Hospitali
ya Mama Ngoma, Mwenge jijini Dar, Jumamosi iliyopita ambako wasanii
walikusanyika kuuchukua mwili wa Kuambiana na kuupeleka Hospitali ya
Taifa Muhimbili gumzo lilikuwa ‘kumbe Kuambiana alikuwa na mke!’
Ni baada ya mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Janeth Rithe
ambaye ni Diwani wa Kunduchi kwa tiketi ya Chadema kufika akiwa analia.
Ilibainika kuwa, mwanamke huyo ndiye mke wa ndoa wa Kuambiana na
walizaa mtoto mmoja .
Kuibuka kwa Janeth kuliibua maswali kutoka kwa wasanii mbalimbali
wakiwemo wadau wa filamu ambao pia walikuwepo. Wengi walijiuliza
ilikuwaje marehemu alitangaza ndoa na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Stara
Thomas mwaka juzi wakati ana mke wa ndoa?
Wengi walisema huenda walitaka ‘kiki’ ya sanaa kwani licha ya
kuanikwa kwa uhusiano wao pia Stara alikuwa akitangaza kutoa albamu yake
ya Injili iliyojulikana kwa jina la Nani ni Mshamba?
Kufuatia gumzo la
uhusiano huo, juzi Uwazi lilimtafuta Stara kwa njia ya simu ya mkononi
na kumuuliza kuhusu hilo ambapo alisema:
Ni kweli tulikutana na Kuambiana na tulipanga kuoana. Lakini kuhusu mke yeye aliniambia alimpa talaka. Kwa hiyo alikuwa huru.
Hata hivyo, tulipeana muda wa kusomana tabia. Oktoba mwaka juzi (2012) tulitofautiana kidogo tukavunja uhusiano. Tukawa tuko pamoja kwa ajili ya sanaa tu, hasa filamu
alisema Stara.
Stara aliendelea kuweka wazi kwamba, Jumamosi ya kifo chake, Kuambiana
alimpigia simu saa mbili asubuhi akamwambia anajisikia kuumwa sana.
Alisema anajisikia kuumwa sana, akakata simu hapohapo. Baadaye nikasikia anapelekwa hospitali, mara nikasikia amefariki dunia
alisema
Stara.
Habari zaidi zinadai kuwa,
marehemu alizaa na Janeth mtoto mwenye miaka 6 sasa aitwaye Miriam
lakini ndugu wa marehemu wamedai mtoto huyo si wa Kuambiana huku ndugu
wa mwanamke wakidai ni wa marehemu.
Marehemu
Kuambiana anazikwa leo Jumanne kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar
baada ya kuagwa kwenye Viwanja vya Leaders Club.
Marehemu anakwenda sambamba na marehemu Steven Kanumba kwa siku ya
kufa (Jumamosi), kuagwa (Leaders Club) kuzikwa (Jumanne) na makaburi
(Kinondoni).
Kwa mujibu wa Steve Nyerere, bajeti nzima ya msiba huo ni shilingi
milioni tano na Bongo Movie imebeba jukumu la mazishi kwa asilimia 95
kuanzia jeneza, maji siku ya kuagwa Leaders na kaburi.
0 comments:
Chapisha Maoni