Habari ya mjini ni maandalizi kabambe ya harusi ya staa wa Bongo Fleva
na Mbunge wa Viti Maalum (CCM) anayewakilisha Vijana Mkoa wa Geita,
Vicky Pascal Kamata ikidaiwa kuwa shughuli hiyo itatafuna kiasi cha Sh.
milioni 96, Ijumaa lina mkanda kamili.Habari kutoka kwa chanzo cha ndani zilisema kuwa Vicky anatarajia
kufunga pingu za maisha Mei 24, mwaka huu na mchumba wake wa muda mrefu
ambaye Ijumaa limemnasa aliyejulikana kwa jina la Charles Pai.
Ilidaiwa kwamba mwanaume huyo ni kigogo ndani ya kampuni moja ya huduma za simu hapa nchini.Kwa mujibu wa mtonyaji wetu huyo ambaye naye ni miongoni mwa wanakamati, harusi hiyo inatarajiwa kuweka rekodi ya aina yake Bongo.
Sijawahi kuona harusi ya kifahari kama ya Vicky, itafanyika tarehe 24 mwezi huu, ina siku chache tu, huwezi kuamini mambo yote yamekamilika
alisema mpashaji wetu.
Imesemekana kwamba baada ya
ndoa hiyo kufungwa kanisani, shughuli itahamia katika hoteli yenye
hadhi ya nyota tano ya Hyatt Regency, The Kilimanjaro iliyopo Posta, Dar
ambapo waalikwa watagonga mnuso wa maana na vinywaji vya kumwaga.Habari zilieleza kuwa sherehe hiyo itahudhuriwa na mawaziri, wabunge
wenzake, vigogo mbalimbali serikalini na baadhi ya wasanii wenzake.
Ilidaiwa kuwa bajeti ya shughuli hiyo imefikia kiasi hicho kwani Vicky anataka iwe ya aina yake.
Kwa mujibu wa mwanakamati huyo,
kwa bajeti hiyo ya Sh. milioni 96, Vicky atakuwa amevunja rekodi ya ndoa
za mastaa zilizowahi kufungwa Bongo.
Ilidaiwa kuwa bajeti ya shughuli hiyo imefikia kiasi hicho kwani Vicky anataka iwe ya aina yake.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Geita, Vicky Pascal Kamata akiwa na mchumba wake Charles Pai. |
Nakwambia harusi ya Vicky haina mfano, itafunika harusi za vigogo na mastaa wengi, itakuwa ya aina yake. Bajeti yake siyo ya kitoto.
Watu wengi wamemchangia, achilia mbali na kuweka hela yake yeye binafsi na mchumba wake, kitu kama Sh. milioni 40.
“Hakika mheshimiwa amejipanga kuvunja ukimya na uvumi mwingi juu ya maisha yake ya kisiasa na jamii inayomzunguka
alisema mtoa habari wetu na kuongeza:
Huwezi kuamini, vikao vingi vya harusi sisi wanakamati tunafanyia Dar. Lakini mara nyingine tunafanyia Dodoma kwa sababu waheshimiwa wengi wanakamati wako huko.
Hata kwenye vikao watu wanakunywa na kula je, siku yenyewe itakuwaje? Unaambiwa msafara wa magari ya kifahari tupu na utakuwa kama wa rais ukiongozwa na farasi.
Baada ya kupata habari hizo,
gazeti hili lilimsaka Vicky kwa udi na uvumba ili kujua mchakato mzima
wa harusi umekaaje lakini simu yake ya mkononi iliita bila kupokelewa
huenda ni kwa sababu ya kubanwa na vikao vya Bunge la Bajeti
vinavyoendelea mjini Dodoma huku bwana harusi akishindwa kutoa
ushirikiano.
0 comments:
Chapisha Maoni