Ijumaa, Mei 16, 2014

KICHAA AUA MTU KWA KUMKATA NA JEMBE KICHWANI MKOANI MBEYA

Mtu mmoja Lackson Kahawa Mwashibanda [66],mkazi wa kijiji cha Masoko Isangati aliuawa kwa kukatwa jembe kichwani na farao adamu [27], mkazi wa kijiji cha masoko.
Tukio hilo limetokea tarehe jana majira ya saa 12:30 asubuhi huko katika kijiji na kata ya Masoko, tarafa ya Isangati,wilaya ya Mbeya Vijijini. Marehemu alivamiwa njiani na mtuhumiwa wakati akiwa anaelekea shambani na jembe lake kisha kumnyag’anya jembe hilo na kumkata nalo kichwani. Mtuhumiwa ambaye anamatatizo ya akili amekamatwa na taratibu za kisheria zinafanywa ili afikishwe mahakamani.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Msangi anatoa wito kwa jamii kuwa na uangalizi maalum kwa watu wenye matatizo ya akili wanaoisha nao ili kuepuka matatizo yanayoweza kuepukika.

0 comments:

Chapisha Maoni