Jumatatu, Mei 26, 2014

JUAN MATA KUONDOKA MANCHESTER UNITED

Meneja mpya wa Manchester United,Louis van Gaal anajiandaa kusikiliza ofa ya Juan Mata kutoka kwa Barcelona waliojiandaa kulipa kiasi cha pauni milioni 40 kwa mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea.
Mata aliyesajili katika majira ya baridi mwezi Januari akitokea Stamford Bridge kwa kiasi cha pauni milioni 37.1,ameonekana kuwa kivutio kikubwa kwa klabu hiyo ya Camp Nou inayotaka kuimarisha kikosi chake mara baada ya kumaliza msimu bila ya taji lolote.
Pia Van Gaal amesisitiza kuwa hayupo katika mipango ya kutaka kusajili Cesc Fabregas kufuatia taarifa zilizosambaa kuwa klabu hiyo ya Old Trafford inajiandaa kupeleka ofa kwa kiungo huyo raia wa Uhispania.

0 comments:

Chapisha Maoni