Jumatatu, Mei 26, 2014

FABREGAS KURUDI UINGEREZA

Klabu ya Barcelona ipo tayari kumuuza Cesc Fabregas kwa kiasi cha pauni milioni 40 katika kipindi hiki cha majira ya joto huku wakitoa ofa kwa Chelsea,Arsenal na Manchester City.
Kiungo huyo ambaye alitakiwa sana na Manchester United mwaka jana kabla ya mashetani wekundu kukataliwa ofa yao,amewekwa sokoni na wanacatalani hao hivyo swali likibaki kuwa ni timu gani itafanikiwa kumnasa raia huyo wa Uhispania aliyewahi kung’aa akiwa na Arsenal katika ligi kuu ya Uingereza.
Arsene Wenger anataka kuhakikisha anamrejesha nyota huyo Emirates Stadium huku akiwa amekabidhiwa fungu la pauni milioni 100 kwaajili ya kuzitumia kwenye dirisha la usajili wa kiangazi.

0 comments:

Chapisha Maoni