Jeshi nchini Nigeria linasema kuwa linajua
wanakozuiliwa zaidi ya wasichana 200 waliotekwa nyara majuma sita
yaliyopita lakini likasema haliwezi kutumia nguvu kuwakomboa.
Afisa wa cheo cha juu jeshini - Mkuu wa Jeshi
Alex Badeh - aliwambia waandamanaji jijini Abuja kuwa hangeweza kufichua
waliko wasichana hao lakini akaahidi kuwa wanajeshi watawarejesha
nyumbani wasichana hao.
Habari nzuri kwa wasichana ni kuwa tunafahamu waliko lakini hatuwezi kuwambia. Hatuwezi kuja na kuwambia siri za kijeshi hapa
mkuu wa wanahewa Alex Badeh aliwambia
waandamanaji jijini Abuja.
Alisema anaamini kuwa watawarudisha wasichana
hao nyumbani hivi karibuni lakini akaeleza masikitiko yake kwa kile
alichosema watu kutoka nje ya nchi wanaochochea ghasia na maandamano.
Bwana Badeh alisisitiza kuw kutumia nguvu kujaribu kuwakomboa wasichana hao ni hatari.
Wapiganaji hawa wanataka kupigana na kwa hivyo wasichana watakuwa hatarini ikiwa kutatokea mkabiliano makali kati ya wapiganaji hao na jeshi la Nigeria
Alex Badeh alisema.
0 comments:
Chapisha Maoni