Jumatatu, Mei 26, 2014

HAKIMU AFUMWA AKIFANYA NGONO NDANI YA GARI IRINGA

KASHFA kubwa idara ya mahakama Iringa ni baada ya hakimu mmoja wa mahakama mjini hapa kufumaniwa ndani ya gari ya mwanamke ambae ni mke wa mpiga picha mmoja maarufu mjini hapa akivunja amri ya sita ndani ya gari nje ya ofisi ya mahakama ya Mwanzo bomani na jirani na ofisi ya mkuu wa wilaya ya Iringa.
Tukio hilo la aibu limetokea usiku wa jana ambapo hakimu huyo ambae anadaiwa kuongoza kwa michepuko na wake za watu alifumwa na njemba lenye mke akiendelea kufungua kurasa za mama huyo ambae pia ni mwalimu wa shule moja za kimataifa katika barabara ya Iringa-Dodoma
Mwandishi wetu alielezwa kuwa mpiga picha huyo maarufu mjini hapa kwa muda amekuwa na mgogoro wa ndoa na mkewe huyo kutokana na mwanamke kuendekeza michepuko na wanaume tofauti tofauti akiwemo hata paroko .

Kutokana na hali hiyo jembe hilo liliamua kufikisha suala hilo mbele ya pirato kwa kutoka ndoa hiyo ivunjike na mahakama hiyo ya mwanzo inadaiwa kuhukumu kimagumashi na hivyo jemba hilo kuamua kusonga mbele zaidi na kesi hiyo kuwa mikononi mwa hakimu huyo aliyefumwa akivunja amri ya sita ndani ya gari.
Hakimu huyo ambae jina lake linaanzia na herufi A baada ya kufumaniwa alilazimika kuendesha gari hilo kwa mwendo kasi kukwepa kichapo huku wakiwa hawajajisitili vema kutokana na nguo zao kuvua ,kabla ya jemba lenye mke kufukuza kwa boda boda na kuungwa mkono na waendesha boda boda ambao walifanikiwa kumkamata hakimu huyo na mama mke wa mtu na kuwapa kichapo kiasi cha hakimu huyo.
Hata hivyo mbali ya kukutwa na mke wa mtu hakimu huyo alikimbilia polisi kufungua kesi ya kimagumashi kuwa eti ameibiwa pesa shilingili laki mbili .

0 comments:

Chapisha Maoni