Jumatatu, Mei 26, 2014

TETESI ZA USAJILI KUTOKA MAGAZETI MBALI MBALI UINGEREZA

Meneja wa timu iliyopanda daraja ya QPR, Harry Redknapp anataka kumchukua kiungo wa Chelsea Frank Lampard na beki wa zamani wa Man U Rio Ferdinand (Sun), Besitkas ya Uturuki inafikiria kumchukua striker wa Chelsea Demba Ba (Daily Mail), Liverpool wametakiwa kuongeza dau hadi paundi milioni 25 kumsajili Adam Lallana kutoka Southampton (Metro), West Ham wamefikia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji Mauro Zarate kutoka Velez Sarsfield (Sky Sports), Tottenham na Juventus zinamtazama kwa karibu mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata ambaye bado hafurahishwi na upangwaji wake (Fichajes.net), Celtic wanafikiria kumchukua meneja wa zamani wa Man U, David Moyes (Mail on Sunday), Tottenham nao wanafikiria kumchukua beki wa zamani wa Chelsea Ashley Cole (Mail on Sunday), Chelsea wameanza kumsaka beki wa Porto Eliachim Mangala (TF1), Samuel Eto'o anataka kwenda Arsenal au Tottenham (The Sun), Barcelona wapo tayari kumuuza Cesc Fabregas kwa paundi milioni 40 na wamewapa nafasi hiyo Chelsea, Arsenal na Manchester City. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.

0 comments:

Chapisha Maoni