Jumapili, Mei 25, 2014

BAADA YA ISABELA MPANDA AOMBA MSAMAHA KWA WATANZANIA BAADA KUVUA NGUO HADHARANI

Baada ya hivi karibuni kuvua nguo na kuonesha sehemu nyeti hadharani, msanii wa muziki na filamu Bongo, Isabela Mpanda ameibuka na kuwaomba radhi Watanzania kwa kitendo hicho kichafu alichokifanya.
Isabela alisema ameumia sana baada ya kuona picha akiwa ameacha sehemu zake nyeti nje hivyo anawaomba Watanzania wamsamehe kwani hakuwa akijua alichokuwa anakifanya kwa sababu ya ulevi.
Naomba Watanzania waliokerwa na kitendo cha kuvua nguo hadharani wanisamehe kwani haikuwa akili zangu wala sikufanya kwa makusudi ila pombe ndizo zilizoniponza
alisema Isabela.
Isabela aliacha nje sehemu nyeti katika kitchen party ya Vanitha Omary iliyofanyika hivi karibuni katika Ukumbi wa Mawela, Dar.

0 comments:

Chapisha Maoni