Jumapili, Mei 25, 2014

MALAWI KUHESABU UPYA KURA LEO

Nchini Malawi kura za uchaguzi mkuu zinatarajwa kuhesabiwa upya hii leo katika maeneo ambapo imedhihirika kuwa idadi ya wapiga kura haiwiani na idadi ya wale waliojiandikisha kupiga kura.
Uchaguzi mkuu wa Malawi umezidi kuchukua sura mpya baada ya wanasiasa na wanasheria nchini humo kupeleka malalamiko yao mahakamani, na kuzidi kuchelewesha matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika jumanne iliyopita.
Kulingana na mwandishi wa idhaa ya Kiswahili ya BBC aliye mjini Lilongwe, Baruan Muhuza, hali nchini humo imekuwa ya sintofahamu ambapo hakuna ye yote anayejua uchaguzi utaishia wapi.
Anasema kuwa tume ya uchaguzi imekiri kuwa kuna maeneo kadhaa ambayo kuhesabu kwa kura kutarudiwa kwa sababu kura zilizopigwa zinazidi waliojisajili.
Tume ya uchaguzi inasema kuwa kuna maeneo mengine ambako watu wamepiga kura mara tatu au mara nne kama vile mji wa Mangochi waliosajiliwa ni watu 39,000 pekee lakini kura zilizopatikana hapo ni 180,000
Baruan alisema.

0 comments:

Chapisha Maoni