Alhamisi, Mei 01, 2014

AKUTWA MTUPU MTARONI

Mtu mmoja ambaye hakufahamika jina lake mara moja, amekutwa akiwa amelala mtaroni maeneo ya Mitandi - Lindi Mjini.
Mtu huyo ambaye ilifahamika ana undugu na mtu mmoja aitwaye "BUSHIRI" katika maeneo hayo alikutwa majira ya saa 2 asubuhi akiwa amelala usingizi mzito mtaroni akionekana na michubuko kadhaa usoni.
Hata hivyo jamaa aligoma kupigwa picha baada ya waandishi wa habari kutaka kumpiga picha licha ya kumweleza kuwa walihitaji kumsaidia kumpata mtu aliyemchukulia nguo zake.
Mashahidi wa tukio hilo lililotokea jana asubuhi walisimulia kuwa mtu huyo ambaye alionekana amelewa baada ya kuamka, alikutwa akiwa amelala fofofo na baada ya kusikia sauti za watu wakimshangaa ndipo alipozinduka na kujikuta YU UCHI na kuzuga kuwa anatafuta msala wa kujisaidia.
Mashahidi hao walisema hawajui zaidi ya nini kilichompata hali iliyomweka katika hali hiyo "isiyoeleweka" kama ametendwa na wahuni ama amelipishwa pombe aliyokunywa.

0 comments:

Chapisha Maoni