Waziri wa Mambo ya Ndani wa Nigeria amesema
kuwa nikutoitendea haki serikali kwa kuilamu kuwa haikufanya chochote
kuwaokoa wasichana wapatao mia mbili waliotekwa.
Wanajeshi wa Nigeria wakiwasaka Boko Haram |
Waziri Abba Moro amesema;
Nigeria imefanya kila linalowezekana kuwaokoa wasichana hao lakini inatokana na unyeti wa operesheni yenyewe japo hakufafanua kwa undani unyeti wenyewe.
Maoni ya Waziri huyo yakakuja wakati mamia ya
wanaigeria hasa wanawake waliamua kuandamana katika mji mkuu wa Abuja
wakishinikiza hatua zaidi kuchukuliwa na serikali ili kuwaokoa wasichana
hao.
Wasichana hao walitekwa wiki mbili zilizopita
wakiwa katika mabweni ya shule iliyopo Kaskazini mashariki na kundi
linalosaidikiwa kuwa ni wapigani wa Kiislamu wa Boko Haram
0 comments:
Chapisha Maoni