Ikiwa ni simk ya tatu tangu mwanasheria mkuu wa CHADEMA na mbunge wa Singida kaskazini Tundu Lissu awatolee maneno yasiyo mazuri hayati J.K. Nyerere na Chama Cha Mapinduzi CCM kuwa;
Nyerere alikuwa mwongo-mwongo...wamezoea vya haramu, vya halali hawaviwezi,
Sasa yasome maneno 134 aliyoiambia Fichuo Tz hivi punde...
Hatukwenda Dodoma Kutafuta POSHO, maana tulikuwa tayari kuifanya Kazi hii ya wanyonge bure bila hata senti, jambo ambalo machumia Tumbo ya CCM hayaliwezi hata chembe. Hatukwenda Dodoma Kuandaa RASMU yenye misimamo ya Makundi na Vyama, maana tayari tulikuwa na Rasmu Iliyoletwa mezani na Tume ya Rais tena kwa ridhaa yake Kisheria. Hatukwenda Dodoma Kuibadili MISINGI mikuu ya Rasmu Iliyoandaliwa na Tume ya Rais, maana hili liko wazi kwamba unapouondoa msingi wa Muundo wa Serikali tatu katika Rasmu ya Tume, ni dhahiri kwamba unakuwa umedhamiria kuifumua Rasmu nzima, hivyo Itakulazimu uanze Mchakato upya, kitu ambacho hatuko tayari kukiona kamwe. Hatukwenda Dodoma Kutukanwa, Kudharirishwa, Kubezwa na hata Kufokewa na VIONGOZI waandamizi wa Serikali tena bila Sababu za msingi ili hali tunao Watanzania mamillioni kwa mamillioni wanaotuunga mkono... CCM na Vibaraka wao, kwa kuwa wameyakoroga, wasiyaone machungu kunywa hekima na busara zitawale!
0 comments:
Chapisha Maoni