Usiulize ni kwanini hii nimeamua kuifanya stori kwako, hii ni kutokana na maisha ya mastaa wengi waliofanikiwa kusahau asili au maisha yao waliyokulia, mfano mzuri ni kwa mastaa wa hapa kwetu Tanzania, wakipata pesa kidogo basi hata life style zao wanabadilisha...hapa naongelea vyakula wanavyokula, nguo hata maongezi pia.
Sasa hii imekuwa ni kinyume sana kwa mwanamuziki chipukizi kutoka nchini Nigeria ambaye pia ni staa wa nyimbo za Skelewu na Aye namwongelea 'Omo baba olowo' Davido ambaye pamoja na mafanikio aliyoyapata bado anapenda kula chakula cha asili, kama ulikuwa hujui ni kwamba Davido anapenda kunywa 'garri' huu ni uji ambao huchanganywa na maharage yaliyochemshwa!!!
Kweli unaweza kushangaa, lakini ndivyo ilivyo na mwenyewe anasema mwanamke akimtaka pia aweze kunywa garri na sio mambo ya fast food..
0 comments:
Chapisha Maoni