Kaka wa wanamuziki mapacha wanaofanya vizuri katika game ya muziki duniani kutoka nchi inayosumbuliwa vilivyo na kundi la wanamgambo wa Boko Haram, Nigeria, P-Square anayefahamika kwa jina la Jude Okoye ambaye pia na manager wa wanamuziki hao na director wa kazi zao amefunguka vilivyo kuhusiana na tetesi za kundi la P-Square kuvunjika ambazo pia nilikupatia habari zake jana.
Taarifa za kuhusu kuvunjika kwa kundi hilo zilitokana na tweet aliyoipost Jude Okoye kama ifuatavyo (Nimeitafsiri kutoka katika lugha ya kiingereza aliyoitumia);
Baada ya miaka 10 ya kazi ngumu, sasa yamekwisha, nimemaliza
Sasa kutokana na hilo siku ya leo asubuhi Jude Okoye amezipinga fununu hizo na kudai kuwa ni mbinu tu za waandishi wa blogu mbalimbali ili kujipatia wasomaji wengi, nanukuu alichokisema hapa
I am too busy to give some wanna be blogger traffic, I don’t know where
that report is coming from. Maybe they just want to get traffic to their site. It’s baseless and untrue.
0 comments:
Chapisha Maoni