Jumatatu, Aprili 14, 2014

SERIKALI IMEONESHA HATI YA MUUNGANO, ITAFUTWE SABABU NYINGINE SASA

Hatimaye serikali imeonyesha hati halisi ya muungano na kusema kuwa ipo tayari kuiwasilisha katika bunge maalum la katiba kama mwenyekiti wa bunge hilo ataona inafaa kufanya hivyo.
Akizungumza na  wandishi wa habari  katibu mkuu kiongozi  Mh Ombeni Sefue amesema serikali  imesikitishwa sana kuona wapo baadhi ya watu wanaodhiriki kusema kuwa hati hiyo haipo .
Akasema  pia  kwamba  ni kwa  busara  za  mwenyekiti  wa bunge maalum l katiba akiona kuna haja ya  hati  hiyo kupelekwa  katika  bunge  maalum   serikali  ipo  tayari.
Aidha  akasema  kuwa   zipo  hati  ambazo  serikali  inazihifadhi kwa umakini  mkubwa   ili kuhakisha  kuwa  zinaendelea  kubaki  salama kwa kizazi cha sasa na kizazi  kijacho.
Kiongozi huyo akaongezea kuwa ni matumaini ya serikali  kuwa  baada  ya  kuitoa  hati hiyo hadharani    watu wataendelea  na mambo ya  msingi yaliyopo mbele yao na siyo kuendeleza malumbano  ambayo  hayana tija kwa  taifa.

0 comments:

Chapisha Maoni