Vincent Kigosi ‘Ray The Greatest’ amefunguka kuwa hana mpango wa kumuoa
mwanadada Chuchu Hans kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.
Akijibu swali aliloulizwa na wanahabari wetu hivi karibuni, kuhusiana na
kudaiwa kuwa baada ya mpenzi wake huyo kupewa talaka ana mpango wa
kufunga naye ndoa kama ilivyokuwa inadaiwa ambapo alikataa katakata
suala la yeye kufunga ndoa na Chuchu.
“Sina mpango wa kuoa ndugu yangu, hayo ni maneno ya watu ambayo yapo tu
mitaani ila kwa sasa niko njiani naenda gym baadaye nitakutafuta
tuongee.” alisema Ray.
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa muigizaji huyo kufunguka kuhusiana na
suala la ndoa na swali linakuja, je, Chuchu anafahamu kuwa anachezewa
tu? Jibu analo mwenyewe moyoni mwake.
0 comments:
Chapisha Maoni