Jumanne, Aprili 15, 2014

FERRY YENYE WATU 460 IMEZAMA KOREA KUSINI, JITIHADA ZA UOKOZI ZINAENDELEA

Oparesheni ya uokozi inaendelea kufuatia ishara za dharura zilizoripotiwa kutoka meli moja ilioyobeba takriban abiria 460 katika pwani ya Korea Kusini.
Maafisa wanasema kuwa walinzi wa pwani hiyo, meli za wanamaji wa Korea pamoja na ndege za uokoaji , zimepelekwa katika ferry moja inayozama kusini mwa pwani hiyo.
Ferry yenye abiria 460 ikizama Korea Kusini.
Shughuli zinaendelea hivi sasa kuokoa zaidi ya abiria 460 wa ferry hiyo .
Jeshi la wanamaji likishirikiana na maafisa wanaolinda usalama katika bahari ya rasi ya Korea.
Maafisa wanasema walipokea habari kuwa meli hiyo imepata matatizo ikiwa imebeba idadi kubwa ya wanafunzi ikitoka Incheon iliyoko kwenye visiwa vya kifahari vya Jeju .
Waokoaji wamewanusuru tayari abiria 160 huku wengine waliosalia wakishauriwa waruke baharini iliwaokolewe.
Walioshuhudia wanasema kulisikika kishindo kikubwa kabla ya ferry hiyo kuanza kusakama maji zaidi ya kilomita 20 kutoka ufukweni.
Shughuli ya uokoaji bado inaendelea huku duru zikidhibitisha kuwa mtu mmoja amepatikana ameaga dunia.

0 comments:

Chapisha Maoni