Kaimu rais wa Ukraine Olexander Turchynov amesema
kuwa vikosi vya kijeshi vya Ukraine vimeuteka na kuuthibiti uwanja mmoja
wa kijeshi katika eneo la Kramatosk mashariki mwa Ukraine,baada ya
mapigano na makundi yanayounga mkono Urusi.
Opresheni dhidi ya ''ugaidi'' yaanza Ukraine |
Rais huyo ameliambia bunge la taifa huko Kiev kuwa operesheni hiyo maalum inafanywa hatua kwa hatua .
Bwana Turchynov aliliambia bunge kuwa operesheni
ya kukomboa miji na mali ya umma kutoka mikononi mwa ''Mgaidi''
itaendelea kuambatana na sheria za kibiniadamu.
Mamia ya watu wanaodaiwa kuwa wanaharakati
wanaounga mkono Urusi wamekongamana nje ya uwanja huo wakiwafokea
majeshi waliotua humo kutoka Kiev.
Makundi ya waasi wanaounga mkono Urusi wameteka takriban miji 10 katika mashariki mwa taifa hilo .
Duru kutoka Marekani zinasema kuwa maelfu ya
majeshi ya Moscow yamezingira maeneo ya mpaka wa Ukraine na kuibua hofu
ya uvamizi wakati wowowte iwapo Ukraine itaingilia kati katika miji hiyo
iliyotekwa.
Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema kuwa
Ukraine huenda ikatumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe iwapo
kiev itaendelea na operesheni hiyo dhidi ya wananchi wake waasi.
Opresheni dhidi ya ''ugaidi'' yaanza Ukraine |
Taarifa kutoka Kremlin zinasema kuwa Putin
alitoa tahadhari hiyo katika mazungumzo ya simu na Kiongozi wa Ujerumani
bi Angela Merkel.
Viongozi hao wanasemekana kuafikiana kuhusiana
na umuhimu wa mkutano wa kwanza wa pamoja baina ya Bara Ulaya Urusi
Ukraine na Marekani.
Mkutano huo unatarajiwa kufanyika huko Geneva Uswisi.
Miji iliyoko Mashariki mwa ukraine zinataka kura
ya maoni kufanyika huko kuamua iwapo wanataka kuendelea kuwa sehemu ya
Ukraine ama wangependa kuiga mfano wa Crimea iliyoamua kujitenga na
kujiunga na Urusi baada ya
utawala mpya kumng'oa madarakani aliyekuwa rais wa nchi hiyo Victor Yanukovich .
0 comments:
Chapisha Maoni