Ijumaa, Aprili 18, 2014

PAMOJA NA KUUGUA KIHARUSI, RAIS ABDELAZIZ BOUTEFLIKA AMECHAGULIWA TENA KUIONGOZA ALGERIA

Taarifa kutoka nchini Algeria zinasema kuwa Rais Abdelaziz Bouteflika ameshinda uchaguzi mkuu uliofanyika mnamo siku ya Alhamisi.
Bouteflika alishinda uchaguzi huo kwa asilimia 80 ya kura na kupata nafasi ya kuongoza kwa muhula wa nne.
Hata kabla ya matokeo kutangazwa, kiongozi wa chama rasmi cha upinzani Ali Benflis, alisema kuwa uchaguzi huo ulikumbwa na wizi.
Bouteflika, ambaye amekuwa mamlakani kwa miaka 15, anakumbwa na hali mbaya ya kiafya kwani anaugua kiharusi na alipiga kura akiwa katika kiti cha magurudumu.

0 comments:

Chapisha Maoni