Ijumaa, Aprili 18, 2014

KUNDI LA P SQUARE LIMEVUNJIKA! KAKA YAO AMETWEET MANENO MAKALI KUHUSU KUNDI HILO

Kuna hofu kubwa sana imetanda baada ya hali isiyokuwa nzuri kulikumba kundi la muziki kutoka Nigeria, kundi la wanafamilia na mapacha la P Square linalowajumuisha Peter na Paul Okoye.
Kutokana na hali iliyopo sasa kuna kila dalili ya tatizo kubwa ndani ya kundi hilo, kaka yao mkubwa ambaye pia ni Manager na muongozaji wao Jude Okoye kupitia mtandao wa kijamii wa Tweeter ametweet maneno haya kama ninavyomnukuu "After 10 years of Hard Work, Now its Over , Am Done...(Baada ya miaka 10 ya kazi ngumu, sasa yamekwisha, nimemaliza...)" Hakuna maelezo ya zaidi kutoka kwao kuhusiana na taarifa hiyo, lakini kutokana na wao wenyewe kama familia pia, Linda, Peter na Paul Okoye wa P-Square imeonekana kuwa kumekuwa na mikwaruzano ya ndani ya kundi.
Kwa muda sasa mapacha hao wa P-Square wamekuwa wakipishana sana katika nyimbo, video na hata mawazo wakati mwingine, lakini kwa taarifa zilizokuwa zimejificha ni kwamba kaka wa mapacha hao Jude Okoye amegombana na wanamuziki hao wakati wakiwa katika mazoezi ya kazi zao siku ya jumatano ya tarehe 16/04/2014 na hata kufikia hatua ya kuwatenganisha madancer wao.
Kuna data za chini sana pia nimezipata kwa mmoja kati ya wake wa mapacha hao ndiye amekuwa chanzo cha malumbano kati ya ndugu hao. INASIKITISHA!

0 comments:

Chapisha Maoni