Ijumaa, Aprili 11, 2014

NYOTA YAKO LEO JUMAMOSI TAREHE 12/4/2014

PUNDA- ARIES (MACH 23- APR 20)
Leo kuna dalili ya mambo yako kukuendea vizuri lakini utajikuta unakabiliwa na kesi ijapokuwa kesi hiyo utakuja kushinda hapo baadae. Yule rafiki yako au ndugu yako aliyekuwa jela atatoka hivi karibuni, lakini atakuletea matatizo makubwa.
NG’OMBE – TAURUS (APR 23 – MAY 20)
Leo huko uendako utakumbana mambo ya kufurahisha au kutatokea hali ya makubaliano na mtu uliyemkopa.Unashsuriwa baada ya matatizo haya usijaribu kukopa tena wuiki hii unaweza kushiondwa kulipa.

MAPACHA - GEMINI (MAY 23- JUN 23)
Wiki hii yule adui yako atakutembelea na kukuudhi.naikitokea ukikutana na mtu mzigo wa aina yeyote, basi elewa kuwa utaona mambo ya ajabu katika matembezi yako utakayoyafanya jioni ya kesho,

KAA - CANCER (JUN 22- JUL 22)
Elewa kwamba huyo unayemfuata huko unakokwenda amepanga kukudanganya, ni vyema usiende. Wiki hii ukimwona mtoto amelala kwenye godoro nje ya nyumba, basi ujue hiyo ni dalili kwamba kuna ugomvi unakuja na kutakuwa hakuna maelewano yeyote mtakayoyafikia,

SIMBA - LEO (JUL 23 –AUG 22)
Matatizo yako ya kifedha yaliyokuwa yanakuandama wewe mwenyewe au familia yako yatakwisha.Kuna mpango utaletewa ambao utakukwamua katika ukwasi. Na ikiwa wiki hii utakutana na mwanamme kabeba Ndoo, hiyo ni dalili kwamba matatizo yako yatakwisha kabisa.

MASHUKE - VIRGO (AUG 23- SEPT 23)
Wiki hii mambo yako mengi yatakuwa hadharani, yatakufedhehesha na kukuaibisha sana, unashauriwa kuwa makini na kila unalotaka kulifanya. Na ikitokea ukimuona mtu ameshika Panga, hiyo ni dalili kwamba utaaibika

MIZANI - LIBRA (SEPT 24- OCT 23)
Leo ukikutana na mtu ambaye Sharubu mchanganyiko nyingi basi ujue kuwa mambo yako utakayo yafanya kwa ushauri wa rafiki yako yatakuwa mabaya, Elewa rafiki huyo ni adui na hatakusaidia .Jiepushe naye.

NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Mambo yako yanahitaji ujasiri wa hali ya juu kuweza kuyaendeleza, ulegevu kidogo tu utakusababishia hasara kubwa usiyoitegemea. Jaribu kuwa mkali na ufatilie kwa karibu mipango yako yote.

MSHALE - SAGITARIUS ( NOV 23 - DES 23)
Leo hii katika shughuli zako za kawaida ukikutana na Mlevi, hiyo ni dalili kwamba kuna safari ya mbali na yenye faida itakujia. Ukipata nafasi hiyo usiiachie.

MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Mambo utakayoambiwa Leo hii yatakuwa ya kweli Hakikisha kila neno unaloambiwa unalifanyia kazi hasa masuala yanayohusiana na mapenzi na biashara. Usiyapuuzie hata kidogo

NDOO –AQUARIUS (JAN 23 – FEBR 19)
Leo kula kila dalili kuwa mambo yako yatafunguka na mikwamo ya hapa na pale itapotea, baada ya muda hali itaendelea kuwa nzuri na matatizo yaliyokujia kwa kasi yatapotea na kukuacha ukiwa na furaha.

SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Siku ya leo mipango yako itakuwa mizuri. Epuka kupingana pingana na watu unaofanya nao Biashara, Jihadhari na marafiki zako inaonekana wiki hii watakujia na mpango ambayousipokuwa makini itakupotezea pesa.

0 comments:

Chapisha Maoni